Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MKWANJA: Mastaa wa soka wanazidi kupiga pesa ndefu duniani

PARIS, UFARANSA. JARIDA la France Football limetoa orodha ya wanasoka wanaolipwa pesa nyingi duniani, huku supastaa wa Barcelona, Lionel Messi akiendelea kushika namba moja kwa mkwanja kwenye mchezo huo. Licha ya kwamba Messi hajashinda Ballon d’Or tangu 2015, staa huyo wa Argentina anavuna kiasi kikubwa cha pesa kuliko hata Cristiano Ronaldo, ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka 2016 na 2017, wakati mshindi wa tuzo hiyo wa mwaka 2018, Luka Modric hata kwenye orodha ya wakali 20 wanaolipwa kibosi kwenye soka hayumo.

Kitu cha kushangaza, wachezaji wenzake kiungo huyo huko Real Madrid, Gareth Bale, Toni Kroos na Sergio Ramos wote wameingia kwenye orodha hii ya wanasoka 20 wanaoongoza kwa kuvuna pesa nyingi duniani. Kipato hicho kimetokana na kiasi walichovuna kupitia mishahara, bonasi na mapato ya matangazo ya kibiashara waliyofanya tangu mwa mmoja nah ii ndio orodha ya wanasoka wenye vipato vikubwa.

20. Sergio Ramos

Klabu: Real Madrid

Kipato: Dola 25.8 milioni.

19. Paul Pogba

Klabu: Manchester United

Kipato: Dola 26.1 milioni.

18. Hulk

Klabu: Shanghai SIPG

Kipato: Dola 26.2 milioni.

17. Kevin De Bruyne

Klabu: Manchester City

Kipato: Dola 26.3 milioni.

16. Sergio Aguero

Klabu: Manchester City

Kipato: Dola 27.2 milioni.

15. Oscar

Klabu: Shanghai SIPG

Kipato: Dola 27.2 milioni.

14. Kylian Mbappe

Klabu: Paris Saint-Germain

Kipato: Dola 28 milioni.

13. Mesut Ozil

Klabu: Arsenal

Kipato: Dola 28.9 milioni.

12. Toni Kroos

Klabu: Real Madrid.

Kipato: Dola 29.5 milioni.

11. Gerard Pique

Klabu: Barcelona

Kipato: Dola 30.3 milioni.

10. Luis Suarez

Klabu: Barcelona

Kipato: Dola 31.4 milioni.

9. Ezequiel Lavezzi

Klabu: Hebei China Fortune

Kipato: Dola 31.7 milioni.

8. Philippe Coutinho

Klabu: Barcelona

Kipato: Dola 33.6 milioni.

7. Alexis Sanchez

Klabu: Manchester United

Kipato: Dola 34.4 milioni.

6. Andres Iniesta

Klabu: Vissel Kobe

Kipato: Dola 37 milioni.

5. Gareth Bale

Klabu: Real Madrid

Kipato: Dola 45 milioni.

Getty

4. Antoine Griezmann

Klabu: Atletico Madrid

Kipato: Dola 49 milioni.

3. Neymar

Klabu: Paris Saint-Germain

Kipato: Dola 102 milioni.

2. Cristiano

Ronaldo

Klabu: Juventus

Kipato: Dola 126 milioni.

1. Lionel Messi

Klabu: Barcelona

Kipato: Dola 145 milioni.