Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miss Tanzania 2024 yanukia

Muktasari:

  • Mchakato wa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2024 utaanza rasmi mapema Januari na kumalizikia Julai mwakani kwa mujibu wa kalenda  iliyotolewa na waandaji.

Waandaaji wa mashindano ya Urembo nchini (Miss Tanzania), kampuni ya The Look imezindua kauli mbiu ya urembo na uongozi ikiwa ni harakati za msimu mpya wa shindano hilo msimu ujao.

Kauli mbiu hiyo ndiyo itatumika kwenyte mashindano ya Miss Tanzania 2024, ikilenga kuwaanda warembo kuwa viongozi bora na kusaidia Taifa katika nyanja mbalimbali.

Mkurugenzi wa The Look, Basilla Mwanukuzi amesema mashindano hayo yamekuwa na ushawishi mkubwa na kumtengeneza mrembo kuwa kiongozi na mtu maarufu na msaada kwa jamii yake tofauti na dhana iliyojengeka miaka ya nyuma kuwa urembo ni uhuni.

"Kauli mbiu yetu kwenye mashindano ya 2024 itakuwa ni urembo na uongozi, ambayo inakwenda kuonyesha fursa zilizopo katika mashindano ya urembo," alisema Basilla aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1998.

Mbali na uzinduzi huo, pia waandaaji wa shindano hilo kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) iliendesha semina kwa Mawakala wa shindano hilo.

Mawakala kutoka mikoa mbalimbali, kanda  na vituo vya Dar Indian Ocean, Temeke, Pwani, Singida, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Kanda ya Vyuo Vikuu.Kanda ya Kati, Kanda ya DSM

 Afisa Sanaa Mwandamizi wa Basata,  Agustino Makame amepongeza Kampuni ya The Look kwa kuendesha mashindano hayo kwa takribani miaka mitano  na kubadilisha maisha ya wasichana wengi.

Amesema mashindano hayo ni sehemu ya kuibeba sura ya nchi kwani mshindi wa Miss Tanzania anakwenda kuitangaza nchi katika mashindano ya urembo ya Dunia. (Miss world) hivyo warembo hao wanatakiwa kujua wameibeba dhamana kubwa ya Taifa.

Katika hafla hiyo, waandaaji waliitumia pia kuwatambulisha baadhi ya wadhamini ambao watadhamini shindano hilo kwa mwaka 2024 ambao ni Kampuni ya It’s All About Cards, Golden Tulip Hotel  pamoja na Wakala wa Misitu Tanzania – TFS