Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mirambo: Mimi na Ninje! Tuko freshi tu

Muktasari:

Huku akicheka, Mirambo alisema katika hali ya kawaida binadamu lazima wakubali kutofautiana ili mambo yaende sawa, lakini si kama ambavyo watu wamekuwa wakizungumza.

KOCHA wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amevunja ukimya kuhusu tetesi za kutoelewana na bosi wake, Ammy Ninje.

Tangu Ninje alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kulikuwepo na tetesi za chini chini kuwa kigogo huyo haelewani na Mirambo.

Huku akicheka, Mirambo alisema katika hali ya kawaida binadamu lazima wakubali kutofautiana ili mambo yaende sawa, lakini si kama ambavyo watu wamekuwa wakizungumza.

“Mimi nipo wazi katika kila jambo, huenda labda ndiyo sababu imefanya watu watafsiri hivyo, lakini naelewana sana na bosi wangu,” alisema Mirambo.

Alisema amekuwa akiripoti kwa Ninje na ni mtu ambaye ana uzoefu wa kutosha katika mpira kwani amefanya kazi nchi ambayo yeye Mirambo ana ndoto za kufikia levo yake.

“Ninje ana uzoefu wa kutosha, amefanya kazi ya soka katika nchi ambayo nina ndoto za kwenda, hivyo nahitaji kujifunza zaidi kupitia yeye,” alisema Mirambo na kufafanua.

“Naelewana sana na bosi wangu, hiyo ya kwamba yeye akienda kulia mimi naenda kushoto ni mitazamo tu, si kweli, wote tunafanya kazi kwa maslahi ya Taifa na tumekuwa tukishirikiana bega kwa bega kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri kwenye Afcon,” alisema.