Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mirambo aomba radhi, agoma kujiuzulu

Muktasari:

  • Timu hiyo ya taifa ya vijana ya Tanzania ilikuwa Kundi A sambamba na Nigeri na Angola zilizofuzu nusu fainali pamoja na Uganda; na kuchemsha vibaya ikiburuza mkia ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haikuambulia hata pointi moja kati ya timu nane zilizoshiriki michuano hiyo ya 13.


HAJA ya mja kunena muungwana vitendo. Saa chache tu baada ya Serengeti Boys kuaga kwa aibu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) U17, Kocha wa kikosi hicho, Oscar Mirambo amewaomba radhi Watanzania kwa kushindwa kutimiza kile alichokiahidi, lakini akigoma kuachia ngazi kikosini.

Mirambo amesema anajua Watanzania wameumizwa sana na matokeo iliyopata Serengeti na kwa kuwa aliwaahidi kufanya mazuri kabla ya kufanyika kwake anawaomba radhi.

“Mimi kama nahodha niliyekiongoza chombo kwa muda wote, napenda kuwaomba radhi Watanzania. Kuna vitu ambavyo tumejifunza kama benchi la ufundi na pia kama nchi. Tulifanya maandalizi ya kutosha lakini kulingana na michuano ilivyo yameonyesha hayakutosha,” alisema.

Kutokana na matokeo mabaya aliyoyapata na kufanya timu yake kuruhusu idadi kubwa ya magoli 12, Mirambo alisema hajafikiria kujiuzulu kama wengine wanavyoshinikiza badala yake analiacha suala hilo mikononi kwa mabosi wake kuamua hatma yake.

“Tulifanya maandalizi ila hayakusaidia, kama mwalimu inabidi lawama zote zije kwangu. Kuhusu kufukuzwa hilo ofisi ndiyo wataamua. Mimi kama mwalimu nimefanya kile ninachoweza kulingana na maandalizi kuelekea michuano hii,” alisema Mirambo.

Timu hiyo ya taifa ya vijana ya Tanzania ilikuwa Kundi A sambamba na Nigeri na Angola zilizofuzu nusu fainali pamoja na Uganda; na kuchemsha vibaya ikiburuza mkia ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haikuambulia hata pointi moja kati ya timu nane zilizoshiriki michuano hiyo ya 13.

Ilifungwa 5-4, 3-0 na 4-2 katika mechi zake tatu.