Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mirambo alia na CECAFA

Muktasari:

  • Mirambo alisema kilichotokea ni kinyume cha matarajio ya wengi nchini na anaomba radhi kwa hilo lakini anajisikia vibaya zaidi baada ya kuona Uganda nayo imeaga mashindano jambo linalofanya Afrika Mashariki na Kati isiingize timu hata moja hatua ya nusu fainali, fainali na Kombe la Dunia.

KITENDO cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kuondolewa mapema kwenye fainali za Afrika (AFCON U17) kimemuachia simanzi Kocha Mkuu wake, Oscar Mirambo aliyekiri kuwa anawajibika kwa matokeo hayo.

Hata hivyo kocha huyo amefichua kuwa pigo hilo la kuondolewa mapema kwa Serengeti Boys halijamgusa yeye na benchi lake au Watanzania bali ni ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati hasa baada ya timu nyingine kutoka ukanda huo, Uganda nayo kuondolewa mapema.

Mirambo alisema kilichotokea ni kinyume cha matarajio ya wengi nchini na anaomba radhi kwa hilo lakini anajisikia vibaya zaidi baada ya kuona Uganda nayo imeaga mashindano jambo linalofanya Afrika Mashariki na Kati isiingize timu hata moja hatua ya nusu fainali, fainali na Kombe la Dunia.

“Tunajua tumewaumiza Watanzania ambao walikuwa na matarajio makubwa na sisi lakini kuna wakati mambo huenda kinyume na ni lazima tukubaliane kwa hilo na kujipanga upya kwa ajili ya siku za usoni.

“Lakini kwa upande wa ukanda wetu hii inatoa picha kuwa bado soka letu liko chini na tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha mashindano yetu ya kuwania kufuzu fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17, yanakuwa bora na imara ili tuweze kushindana na wenzetu wa kanda nyingine,” alisema Mirambo.

Serengeti Boys na Uganda ambazo zilikuwa kundi moja, zilishindwa kufua dafu mbele ya Nigeria na Angola zilizosonga mbele na kukata tiketi ya kwenda kwenye Kombe la Dunia kwa vijana wa umri huo zitakazofanyika Brazil Oktoba mwaka huu.