Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miloud agusia dabi, wakiikabili Prisons

KIHIMBWA Pict

Muktasari:

  • Tanzania Prisons inatarajiwa kuwa wenyeji wa Yanga mjini Mbeya kesho katika mechi ya Ligi Kuu Bara, ukiwa ni mchezo wa 28 kwa Yanga ilhali ni wa 29 kwa Prisons, lakini mzuka ukiwa ni mkubwa kwa pande zote ambazo kila moja inajiwinda kwa ajili ya kutimiza lengo muhimu msimu huu. Prisons inajiwinda kutoshuka daraja ilhali Yanga ikiutaka ubingwa.

WAKATI Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Amani Josiah akisema kwa muda waliofanya mazoezi vijana wake wameonyesha ari na morali kubwa hivyo kesho matarajio ni kuendeleza matokeo mazuri, yule wa Yanga, Miloud Hamdi amesema wako tayari na fiti kwa ajili ya mechi hiyo, lakini akigusia kidogo kuhusu Dabi ya Kariakoo.

Tanzania Prisons inatarajiwa kuwa wenyeji wa Yanga mjini Mbeya kesho katika mechi ya Ligi Kuu Bara, ukiwa ni mchezo wa 28 kwa Yanga ilhali ni wa 29 kwa Prisons, lakini mzuka ukiwa ni mkubwa kwa pande zote ambazo kila moja inajiwinda kwa ajili ya kutimiza lengo muhimu msimu huu. Prisons inajiwinda kutoshuka daraja ilhali Yanga ikiutaka ubingwa.

Hamdi akizungumza leo, amesema wachezaji wote wapo fiti na kwamba presha ya mchezo wa dabi dhidi ya Simba ambao umevuta hisia nyingi za mashabiki haijaathiri chochote kwa vijana wake.

"Hatuidharau Prisons, hatujaja hapa kufurahisha na kutania tunahitaji pointi tatu na rekodi yetu imekuwa nzuri na hii inanipa matumaini makubwa kesho kuendeleza ushindi," amesema Miloud.

"Kiufundi tuko imara na wachezaji waliobaki Dar es Salaam siyo kwa sababu ya kisaikolojia kuhusu mechi ya dabi, bali ni wagonjwa. Kimsingi tumejipanga kushinda."

Awali, Josiah amesema kinawachotia nguvu Prisons ni matokeo mazuri ya mechi nne zilizopita na kwamba kukutana na Yanga itampa mwelekeo mzuri katika kazi yake.

"Tofauti na timu nyingine kwa nilichofanya kukutana na Yanga ambayo ni kubwa na wachezaji wake itanipa ujasiri na kujua uwezo wangu ukoje. Kimsingi ni mechi muhimu sana katika hali ya kukwepa play off (mtoano)," amesema.

Yanga ndio inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa pointi 73 ikiwaaacha pointi moja watani zake Simba baada ya mechi 27, huku Prisons ikiwa na pointi 30 katika nafasi ya 13 na michezo miwili ili kumaliza msimu huu.

Rekodi zaibeba Yanga 
Katika mechi tano za nyuma, Prisons imeonekana kuwa wanyonge dhidi bingwa huyo mtetezi ikipoteza zote ikiwamo kisago cha mabao 4-0 katika mchezo wa mwisho uliopigwa Desemba 12, 2024.

Hata hivyo, Wajelajela hao wanashuka uwanjani wakiwa na mwendelezo wa matokeo mazuri, ambapo katika mechi nne za mwisho wameshinda tatu na kupoteza moja dhidi ya KMC.

Yanga haijapoteza mchezo wowote kati ya mitano ya Ligi Kuu ambapo mara ya mwisho kupoteza ilikuwa Novemba 4,2024 ilipofumuliwa mabao 3-1 na Tabora United.