Michezo ya ubashiri inavyosaidia kukuza ustawi wa sekta ya fedha

Ukuaji wa sekta ya michezo ya ubashiri umeathiri pia mwenendo wa sekta ya fedha nchini, ni sarafu za pande mbili kwa lugha sahihi. Unahitaji rasilimali fedha kuweza kufanya ubashiri na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda fedha nyingi.
Kwa kawaida, madau yanayotolewa kama zawadi na kampuni za michezo ya kubashiri huwekwa benki kwa sababu za usalama, jambo ambalo limekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia sekta hiyo kupiga hatua.
Fedha hizo za madau ya ushindi zinapowekwa katika benki mbalimbali hutozwa ada na benki hizo ambazo huwa ni kubwa na husaidia benki kukuza mtaji na kuboresha huduma zake kwa wateja kutokana na mzunguko wa fedha kuwa wa uhakika.
Achilia mbali madau ya ushindi, kampuni za michezo ya ubashiri pia hufungua akaunti maalumu kwa ajili ya kutunza fedha zinazokusanywa na wateja wao kwa kuwa ni kiasi kikubwa kinachokusanywa kutoka kwa wadau wa michezo ya ubashiri. Kwa utaratibu huu na wingi wa kampuni hizi za kubashiri nchini, benki pia zinaongeza na kukuza kiwango chake cha amana na wateja wapya.
Haishii hapo, kampuni kubwa za michezo ya ubashiri, kwa kawaida, huingia makubaliano na kampuni za huduma za mitandao ya simu nchini (Vodacom, Tigo, Airtel na Halotel) ili kuwezesha wachezaji wa michezo ya ubashiri kubashiri kupitia simu zao za mkononi ili kuwaondolea usumbufu wa kubeba fedha katika waleti zao na kwenda katika maduka/vituo maalumu vya kubashiria.
SportPesa, kampuni kinara wa michezo ya ubashiri nchini na ambayo imezalisha mabilionea wa kwanza kupitia michezo hiyo, imekuwa na mchango mkubwa katika kusukuma ukuaji wa sekta ya fedha kutokana na ushirikiano wake ulionao na taasisi za fedha na kampuni za mitandao ya simu.
Madau makubwa yanayowaniwa, pale mshindi anapopatikana, huwekwa katika Benki ya CRDB, mshirika wa karibu wa kampuni hiyo katika kutunza amana za wateja wao na zawadi za ushindi (fedha).
Kwa upande wa mitandao ya simu, wateja wote wa SportPesa wanaweza kuweka ubashiri wao kupitia majukwaa ya huduma za fedha za mitandao ya simu ya Vodacom, Airtel, Tigopesa na Halotel.
Endelea kubashiri kupitia tovuti ya www.sportpesa.co.tz