Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda anyoosha maneno Bara

Muktasari:

  • Namungo imemaliza msimu ikiwa nafasi ya tisa baada ya kukusanya pointi 35, imeshinda mechi tisa, sare nane na kupoteza mechi 13 ikifunga mabao 28 na kuruhusu 36.

BAADA ya kukwepa mtego wa kushuka Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa Namungo, Juma Mgunda amesema walikuwa na msimu mbaya, lakini wamegundua walipokosea na sasa wanajipanga kurudi imara 2025/26.

Namungo imemaliza msimu ikiwa nafasi ya tisa baada ya kukusanya pointi 35, imeshinda mechi tisa, sare nane na kupoteza mechi 13 ikifunga mabao 28 na kuruhusu 36.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mgunda alisema walikuwa wamekutana na changamoto nyingi kutoka kwa wapinzani wao kutokana na kutokuwa na kikosi cha ushindani, huku akitaja eneo la ushambuliaji na ukabaji hawakuwa bora na ndio sababu kubwa iliyowaangusha msimu huu.

“Jambo zuri ni kwamba tumejitetea na kujihakikishia kushiriki msimu ujao, hatuwezi kurudi kinyonge tumejifunza na tutajiandaa kuhakikisha tunakuwa timu shindani kwa kufanya maboresho maeneo mengi ambayo hatukuwa vizuri,” alisema.

“Ili uwe bora na mshindani unatakiwa kuwa na wachezaji wenye uchu na mafanikio na pia bora kwa ushindani. Hilo kwenye kikosi chetu lilikosekana hasa eneo la ushambuliaji na ukabaji, tumeruhusu mabao mengi wakati huohuo hatujafunga idadi kubwa ya mabao. Hilo ni tatizo, tutarudi imara msimu ujao.”

Mgunda alisema kilichowatokea msimu huu siyo bahati mbaya na Namungo siyo timu ya kwanza kukutana nayo. “Kitu cha msingi tunapaswa kusahau yaliyopita na tuweke nguvu kwenye ujenzi wa timu bora na shindani msimu ujao ili tusirudie makosa,”” alisema.

“Kukubali kukosea ni hekima, tulikosea tutajipanga na tuna imani kubwa kuwa kama tutatengeneza kikosi kizuri tutakuwa miongoni mwa timu tano bora msimu ujao. “