Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nasser amtisha mtetezi mbio za Rwanda

MAGARI Pict

Muktasari:

  • Rwanda Mountain Gorilla  ndiyo jina rasmi la raundi hii ambayo Mtanzania Nasser atakuwa akiiongoza kwa sababu ya wingi wa pointi.

MTANZANIA Yassin Nasser  ambaye yuko mbele ya bingwa mtetezi Karan Patel wa Kenya kwa pointi 28, anaanza kuliona taji la ubingwa wa Afrika, na azma hii itaamuliwa katika raundi ya tatu ya mbio za magari ubingwa wa Afrika nchini Rwanda mwishoni mwa juma hili.

Rwanda Mountain Gorilla  ndiyo jina rasmi la raundi hii ambayo Mtanzania Nasser atakuwa akiiongoza kwa sababu ya wingi wa pointi.

Nasser ambaye ataongozwa na msoma ramani toka Uganda, Ally Katumba ndani ya gari aina ya Ford Fiesta, anaingia katika raundi hii akiwa na jumla ya pointi 63 wakati bingwa mtetezi Karan Patel ana pointi 35.

Kabla ya kuanza kwa raundi ya tatu, aliyemkaribia Nasser kwa pointi alikuwa Nikhil Sachania  wa Kenya mwenye pointi 50, Carl Tundo, pia wa  Kenya mwenye pointi 50, Jeremiah Wahome (pointi 42) na Samman Vohra (pt36).

 Karan Patel, ambaye ndiye bingwa wa mbio za magari ubingwa wa Afrika kwa mwaka 2024, anakuja Rwanda akiwa na pointi 35 kibindoni, akiwa nyuma ya Mtanzania Nasser kwa pointi 28.

Mbio za Rwanda Mountain Gorilla zitafanyika kuanzia Ijumaa, Julai 4 hadi Jumapili, Julai 6 mwaka huu.

Patel, ambaye anaongozwa na msoma ramani Tauseef Khan wakiendesh gari aina ya Skoda Fabia, ndiye pia bingwa mtetezi wa mbio za Mountain Gorilla.

Kilichofufua matumaini ya Patel ni ushindi wake katika mbio za Pearl of Afrika za Uganda ambao ulimpa pointi 35.

“Tuna nia ya dhati ya kutetea ubingwa wetu wa Afrika ingawa haitakuwa ni kazi rahisi,” amesema Patel katika mahojiano na vyombo vya habari.

Pamoja na nyota wanane wanaogombea ubingwa wa Afrika, kuna madereva 35 waliojiandikisha kushiriki mbio hizi za nchini Rwanda.

Mashindano yatakuwa na jumla ya kilometa 386 yakianzia katika Ukumbi  wa Kigali Convention Center kabla ya kuelekea maeneo ya Bugesera ambako zitachezwa raundi mbili na baada yake kuhamia katika maeneo ya Gako and Nemba.

Prince Charles Nyerere ni Mtanzania wa pili anayeshiriki katika raundi ya tatu ya ubingwa wa Afrika nchini Rwanda.

“Niko tayari kabisa kwa mashindano haya baada ya kushindwa kushiriki raundi ya ufunguzi nchini Kenya kutokana na kuuguliwa na mama mzazi,” amesema Prince. Nyrerere ambaye ni mjukuu wa Baba  wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Prince Nyerere  atamtegemea msoma ramani kutoka Rwanda, Fernand Rutabingwa ambaye anazijua vyema barabara za nchini kwake na changamoto zake.

Prince Nyerere anaingia na gari aina ya Mitsubishi Evolution X ikiwa katika ubora mkubwa.