Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda aibukia kwa vijana Simba

Muktasari:

  • Mgunda ambaye hakusafiri na Simba kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu, amekuwa kwenye sintofahamu kubwa kuhusiana na hatima yake ndani ya timu hiyo inayonolewa na Mbarazili, Roberto Oliveira 'Robertinho'.

HUKO Simba hali sio shwari kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Juma Mgunda baada ya kuonekana akiwa na kikosi cha vijana.

Mwanaspoti limemshuhudia Mgunda akiwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni wakati wa kutafuta vipaji vitakavyojiunga na timu hiyo chini ya kocha mkuu, Selemani Matola na mkuu wa programu za soka la vijana, Patrick Rweyemamu.

Mgunda ambaye hakusafiri na Simba kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu, amekuwa kwenye sintofahamu kubwa kuhusiana na hatima yake ndani ya timu hiyo inayonolewa na Mbarazili, Roberto Oliveira 'Robertinho'.

Taarifa za mwanzo ambazo Mwanaspoti ilizipata ilieleza Mgunda alitakiwa kupewa timu ya Simba Queens jambo ambalo hata hivyo yeye mwenyewe ilielezwa hayuko tayari kufundisha kwa upande huo kwenye soka la wanawake.

Kuonekana kwa Mgunda kwenye soka la vijana kunaibua maswali mengine ingawa hata hivyo viongozi wa Simba bado hawajaweka wazi cheo chake kipya.

Mgunda alijiunga na Simba Septemba 7, mwaka jana akitokea Coastal Union baada ya timu hiyo kuachana na Zoran Maki aliyesitishwa mkataba wake.