Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgogoro wa Iran, Israel wamkwamisha Wazir Jr Iraq

WAZIRI Pict

Muktasari:

  • Wazir Jr ambaye aliwahi kukipiga Yanga msimu wa 2020/21, alijiunga na timu hiyo iliyopo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi yenye timu 20, kwa mkataba wa miezi sita mwanzoni mwa msimu huu na tangu atambulishwe kikosini hapo Februari 5 mwaka huu, hajapata nafasi ya kuanza moja kwa moja kwenye timu hiyo.

MSHAMBULIAJI wa Al Mina’a, Wazir Jr Shentembo amesema mgogoro kati ya Iran na Israel umesitisha safari za ndege kwa timu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Wazir Jr ambaye aliwahi kukipiga Yanga msimu wa 2020/21, alijiunga na timu hiyo iliyopo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi yenye timu 20, kwa mkataba wa miezi sita mwanzoni mwa msimu huu na tangu atambulishwe kikosini hapo Februari 5 mwaka huu, hajapata nafasi ya kuanza moja kwa moja kwenye timu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Wazir Jr alisema msimu umekuwa mgumu kwake pamoja na timu kutokana na kile kinachoendelea Iran na Israel, hasa ndege zinazokatisha nchini humo.

“Mgogoro huo, naweza kusema unaathiri soka nchini humo kwa kiasi fulani, tunatembea umbali mrefu hadi kilomita 1300 kwa basi kutokana na kuzuiliwa kwa ndege,” alisema Wazir Jr.

Alipoulizwa kama ataendelea kusalia kikosini hapo msimu ujao, alisema:

“Mazungumzo yameanza lakini timu zinapenda mchezaji huru kwa sababu hakuna usumbufu. Kama unavyojua nipo kwa mkopo kutoka Dodoma Jiji, ila changamoto kubwa ni kocha aliyenisaini aliondoka.”

“Mbali na mazungumzo hayo, pia sidhani kama nitasalia kutokana na ofa zingine kutoka Uarabuni, timu moja kutoka Ligi Kuu Algeria na Saudia Ligi Daraja la Kwanza kwa hiyo ofa zipo.”