Mchongo wa Mwanaspoti ulivyowatoa kimaisha

Muktasari:
Kwa upande wa Daudi Charles kutoka Mbezi Mpigi Magoe aliyejinyakulia simu aina ya 'Smartphone', alisema hakutarajia kupata zawadi hiyo jambo alilodai hawezi kuliacha kulisoma Mwanaspoti maishani mwake.
PAMOJA na Mwanaspoti kuwa gazeti makini kwa kuchapisha habari za uhakika, pia halijawasahau wasomaji wake ambapo linawapatia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya shinda mchongo.
Washiriki wa shindano la shinda mchongo wa Mwanaspoti wameendelea kujinyakulia zawadi mbalimbali kama bodaboda, simu za mkononi na pesa taslimu Sh 100,000.
Hivi karibuni Giziraly Maliniche kutoka Tandika, Temeke, alijinyakulia zawadi ya bodabodana kufunguka mengi namna mchongo huo ulivyobadilisha maisha yake.
Maliniche alisema alikuwa na maisha ya hali ya chini, kiasi kwamba alikuwa hajui afanye nini, kitendo cha kushinda bodaboda alidai ataitumia kwa ajili ya biashara.
"Mwanaspoti nimeamini ni gazeti la jamii, mbali na umahiri wa habari zao lakini linajali wasomaji wake, kwanza nilikuwa siamini kwamba naweza kupata zawadi ya bodaboda ambayo itainua maisha yangu kiuchumi.
"Nawashauri wasomaji wa habari za michezo, wanunue gazeti la Mwanaspoti litabadilisha maisha yao kama ilivyotokea kwangu, furaha nilionayo nakosa neno la kusema, ila naamini gazeti hilo litabakia kuwa juu,"alisema.
Kwa upande wa Daudi Charles kutoka Mbezi Mpigi Magoe aliyejinyakulia simu aina ya 'Smartphone', alisema hakutarajia kupata zawadi hiyo jambo alilodai hawezi kuliacha kulisoma Mwanaspoti maishani mwake.
"Si jambo dogo nimenunua gazeti 800 napata smartphone ya bei kali, nimeamini Mwanaspoti mbali na kuwajali wasomaji wake kuwapa habari za ukweli pia linawainua kimaisha,"alisema.
Ulusura Mohamedi kutoka Magomeni ni mmoja wa washindi waliojinyakulia pesa Sh 100,000, alisema ameanza kula matunda ya Mwanaspoti ambalo ndilo gazeti lake pendwa la michezo, akiligusia na Mwananchi kwamba ndio anayoyaamini kwa habari za uhakika.
"Nauza genge hiyo pesa imeongezea kwenye mtaji wa biashara zangu ndogo ndogo, nawahamasisha wengine wacheze watapata kwani hata mimi sikutarajia,"alisema.