Prime
Mbeya City vs Mashujaa Juni 24, kiingilio bure

Mechi ya marudiano hatua ya mtoano kutafuta timu itakayocheza Ligi Kuu na Championship msimu ujao kati ya Mashujaa na Mbeya City itapigwa Jumamosi Juni 24.
Ofisa wa Habari Bodi ya Ligi Kuu, Karim Boimanda amesema mechi hiyo ilipangwa kupigwa Juni 24 na sio 22 kama taarifa ilivyosambaa.
"Mechi ya mwisho ya marudiano ya play-off kati ya Mbeya City na Mashujaa itachezwa Juni 24 uwanja wa Sokoine na sio Juni 22 kama inavyoelezwa,"
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametangaza hakutakuwa na kiingilio katika mechi hiyo ili kutia hamasa timu hiyo iliyofungwa jana Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma mabao 3-1 kusaka ushindi ili ibaki Ligi Kuu ila isipofanikiwa itaenda Championship.