Matola awapa U20 mechi ya Mtibwa

Thursday June 23 2022
starts pic
By Ramadhan Elias

KAIMU kocha mkuu wa Simba, Seleman Matola amewapa nafasi wachezaji watatu kutoka kikosi cha U-20 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaoanza saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wachezaji hao ni Hassan, Shafii na Kasimu kutoka timu ya vijana na kwenye mchezo wa leo wataanzia benchi ikiwa ni mara ya kwanza kwa Simba msimu huu kuwapa nafasi wachezaji wa U-20 kwenye mechi ya kimashindano.

Katika kikosi cha wachezaji 11 watakaoanza golini yupo Beno Kakolanya huku Gadiel Michael, Jimmyson Mwanuke, Kennedy Juma na Pascal Wawa wakicheza kama mabeki.

Viungo ni Sadio Kanoute, Erasto Nyoni, na Pape Sakho. Meddie Kagere atacheza eneo la mshambuliaji wa kati, Kibu Denis na Peter Banda watakuwa mawinga.

starts pic 1

Kikosi cha Mtibwa

Benchi wapo Shafii, Hassan na Kasimu wote kutoka U-20 sambamba na Ally Salim, Joash Onyango, Henock Inonga, Taddeo Lwanga, John Bocco na Yusuph Mhilu.

Advertisement

Simba pia itatumia mchezo huo kumuaga beki wake Wawa aliyemaliza mkataba na Wekundu wa Msimbazi hao baada ya kuitumikia kwa misimu mitano mfululizo.Advertisement