Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Yanga wampokea Chama kifalme

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa kimataifa wa Zambia, aliyesajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kumuongezea mwingine, baada ya kuitumikia Simba kwa miaka sita, aliwapa ‘thank you’ juzi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuamsha mzuka kwa mastaa wa timu hiyo mpya waliomsifu kwa kuungana nao.

HUKO Jangwani, unaambiwa sio mashabiki na wapenzi tu wa Yanga waliofurahishwa na ujio wa kiungo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Clatous Chama aliyesajiliwa akitoka kumaliza mkataba na Simba, lakini kumbe hadi mastaa wa timu hiyo wamechekelea usajili huo na kumpokea Mwamba wa Lusaka kifalme.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Zambia, aliyesajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kumuongezea mwingine, baada ya kuitumikia Simba kwa miaka sita, aliwapa ‘thank you’ juzi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuamsha mzuka kwa mastaa wa timu hiyo mpya waliomsifu kwa kuungana nao.

Mastaa watatu wa Yanga wamezungumzia juu ya ujio wa Chama na kusema ni bonge la usajili ambao unaenda kuongeza makali yao kikosini baada ya kufunika kwa misimu mitatu mfululizo katika Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.

Nahodha msaidizi wa Yanga, beki Dickson Job ameliambia Mwanaspoti ujio wa Chama kwenye kikosi chao utakuwa ni sawa na kuwaongezea gia muhimu kutokana na ufundi wake.

Job alisema timu yao itakuwa na watu bora wa kutosha ambao hata kama akikosekana mmoja wengine bora wataziba nafasi yake tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.

“Kila mtu anamjua Chama, kila timu inatamani kuwa naye kwahiyo anapokuja kwetu sisi kama wachezaji wenzake tunamkaribisha na tunaamini atatuongezea kitu kikubwa,” alisema Job na kuongeza;

“Kuna faida nyingi za kuwa na mchezaji kama Chama, kama mnakumbuka msimu uliopita, kuna wakati aliumia Pacome (Zouzoua) tulipata wasiwasi sana lakini kwa sasa anakuja Chama hii inaipa timu uhakika kama huyu akikosekana basi kuna mwingine.

“Kwetu mabeki pia tutakuwa na nafasi ya kupumzika, hakuna kitu muhimu kwa mabeki kama mkipeleka mpira mbele usikae muda mrefu na ukarudi lakini kwa watu tutakaokuwa nao kule mbele itatusaidia sana mabeki.”

Stephanie Aziz KI alisema muda mrefu alitamani kucheza pamoja na Chama ambapo hata alipoulizwa na mabosi wa timu hiyo alijibu kwa haraka aletwe Yanga.

“Chama ni mchezaji mkubwa mwenye kipaji kikubwa, ujio wake Yanga naamini ataleta nguvu kubwa ambapo tutakaposhirikiana Yanga itafanya makubwa, mnapokuwa na kikosi kipana kinawasaidia sana kimataifa na hata ligi ya ndani,” alisema Aziz KI na kuongeza;

“Kuna wakati niliongea na viongozi wetu wa juu wakaniuliza vipi tukimleta Chama, nilijibu kwa haraka aje hata sasa, ni mchezaji niliyekuwa natamani wakati wote kucheza naye.”

Beki Yao Kouassi alisema wakati akikutana na Chama akiwa timu pinzani alikuwa analazimika kujiandaa sawasawa kutokana na ubora wake hasa akiwa anatokea pembeni.

“Nilikutana mara ya kwanza na Chama wakati nikiwa Asec yeye akiwa na Simba, niligundua muda mrefu kwamba anajua sana, ana ufundi mkubwa unahitaji kutuliza akili kukabiliana naye lakini sasa anakuja kwetu nadhani ni mtu bora anayekuja kuongezeka kwenye familia yetu.”

Chama ametua Yanga akiwa ameichezea timu hiyo zaidi ya mechi 170 akiifungia mabao 42 na asisti 60, huku msimu uliopita alihusika na mabao 14 akifunga saba na kuasisti saba.