Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Yanga kuifuata Al-Merrikh Septemba 14

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amezungumzia utaratibu wa usafiri wa timu hiyo na mashabiki kwenda nchini Rwanda kwenye mechi ya hatua ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh katika Uwanja wa Pele Septemba 16.

"Timu inatarajia kuondoka Alhamisi  Septemba 14 kwenda Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kwanza raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh SC,"

"Najua Watanzania wengi wanayo kiu ya kwenda kushuhudia mchezo wetu dhidi ya Al-Merrikh. Klabu imeaanda mpango wa kusafiri na mashabiki kutoka hapa Dar es Salaam kwenda Kigali, Rwanda. Wachezaji na benchi la ufundi watasafiri kwa njia ya anga, mashabiki na viongozi watasafiri kwa njia ya basi"

"Tayari kuna mashabiki wamejaza mabasi mawili ya kakonko huko Kigoma. Nimearifiwa wapo wengine wengi kutoka Kigoma wanafanya utaratibu wa kwenda. Bukoba pia wamejaza basi moja, Mwanza wamejaza basi moja na lingine linakaribia kujaa. Ukichelewa hii fursa usije kutulaumu"

"Tumepokea jumbe mbalimbali kutoka Rwanda wakitusubiria kwa hamu kubwa. Rwanda nzima inayo kiu kubwa ya kutupokea. Misafara yote itaondoka siku moja. Kwa wale wanaotumia basi wataondoka hapa Septemba 14 saa 11 alfajiri, na kwenda kulala Kahama kabla ya kwenda Rwanda. Kurudi itakuwa Septemba 17 au tunaweza kuongeza siku"

"Tutakuwa na mabasi rasmi ambao Uongozi wa Young Africans umeendaa. Kila ambaye anahitaji kwenda atahitajika kutoa kiasi cha Sh150,000 ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi. Utaratibu wa kula kunywa na kulala kila mtu atajitegemea mwenyewe. Hata hivyo kila mtu atapaswa kuwa na hati ya kusafiria"