Mastaa wapya Simba waanza kuuwasha...Yanga, Mbeya City zashuka

Muktasari:
- Ushindi huo ilioupata Simba kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi umeifanya kuzishusha Mbeya City na Yanga kwenye kilele cha msimamo kwa idadi ya mabao.
Wachezaji wapya Simba wameanza Ligi Kuu NBC kwa kishindo baada ya kuisaidia timu yao kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Geita Gold kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ushindi huo ilioupata Simba kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi umeifanya kuzishusha Mbeya City na Yanga kwenye kilele cha msimamo kwa idadi ya mabao.
Awali Mbeya City ndio iliyokuwa ikiongoza msimamo huo kufuatia ushindi walioupata mapema wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji.
Huku Yanga ilishika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao maana wote wamevuna pointi tatu kwenye michezo yao ya kwanza ya msimu.
Mabao ya Simba kwenye mchezo wa leo, yamefungwa na Augustine Okrah, Moses Phiri na Clatous Chama kwa mkwaju wa penalti.
Msimu uliopita Simba ilianza kwa suluhu dhidi ya Biashara ya Mara ambayo ilishuka daraja.
Geita Gold yenyewe imeendeleza rekodi mbovu ya kupoteza kwenye michezo yao ya kwanza, msimu uliopita ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo.
Kikosi cha Simba, Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalal', Hennock Inonga, Mohammed Ouattara, Jonas Mkude, Sadio Kanoute, Pape Sakho, Clatous Chama, Moses Phiri, Peter Banda.
Geita Gold, Sebusebu Samson, Aman Wawa, Yahaya Mbegu, Oscar Masai, Kelvin Nashon, Deusdedith Okoyo, Yusuph Kagoma, George Mpole, Dan Lyanga na Edmund John.