Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa waliopiga pesa nyingi za usajili, posho

KIPINDI kama hiki cha dirisha dogo la usajili ambao kwa kwa sasa kimeangukia kwenye msimu wa sikukuu, baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu Bara wanaishi katika mazingira mazuri kutokana na pesa ambazo wamevuta katika usajili wao pamoja na posho mbalimbali.

Mwanaspoti inakuletea baadhi ya mastaa ambao wamevuta pesa ya maana katika sajili zao lakini posho ambazo wanaendelea kuchukua kutokana timu zao kuibuka na matokeo mazuri katika mechezo mbalimbali ya Ligi Kuu Bara pamoja na michuano mingine.

BERNARD MORRISON

Winga huyu wa Simba alisajiliwa kwa mbwembwe na alitikisa katika vyombo vya habari, vijiwe vya soka na maeneo mengine mbalimbali akitokea Yanga na gharama yake ya usajili ilikuwa ni Dola za Kimarekani 85,000 ambazo kwa pesa ya Kitanzania inakuwa zaidi ya Sh196 milioni.

Baada ya kuvuta mkwanja huo mrefu wa usajili tena kimya kimya alionekana kucheza katika kikosi cha Simba mwanzo wa msimu kama moja ya wachezaji aliyekuwa akiwafurahisha mashabiki wa kikosi hiko kutokana na mambo ambayo alikuwa akiyafanya.

Miongoni mwa raha ambazo Morrison alikuwa akiwapa mashabiki na wapenzi wa Simba ni mabao mawili ambayo alifunga dhidi ya Vital’O ya Burundi na Namungo katika mechi ya ufunguzi wa msimu huku akisababisha penati ambayo John Bocco alikwenda kufunga kwa penalti.

Mabosi wa Simba huwa na utamaduni wa kutoa posho Sh300,000 kwa kila mchezaji ambaye amecheza katika mchezo wa ligi ambao wameshinda, 200,000 kwa wale ambao watakuwa benchi lakini hawakuingia, Sh 100,000 kwa wale ambao hawakuwepo hata katika benchi la akiba.

BAKARI MWAMNYETO

Beki wa kati wa Yanga usajili wake ulikuwa wa vuta nikuvute kutokana na kuhitajika na timu tatu kubwa hapa nchini Simba na Azam ambao walishindwa kumpata kutokana na pesa ambayo ilikuwa inahitajika na mchezaji mwenyewe pamoja na timu yake ya Coastal Union ya Tanga.

Baada ya ushindani huo wa vigogo Yanga walifikia makubaliano na mchezaji huyo kutoa Sh150 milioni ili kumpata Mwamnyeto ambaye kuna pesa yake alichukua ambayo haikuwa chini ya Sh70 milioni na nyingine iliyobaki ilikwenda Coastal Union kutokana alikuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja pamoja na wasimamizi wake.

Yanga msimu huu wamekuwa wakitoa posho kama watashinda mechi tatu mfululizo na wale wachezaji ambao wamecheza ndio wanakuwa katika orodha ya nyota waliopata kipato kikubwa na Mwamnyeto akiwa katika orodha hii kuliko wale ambao hawachezaji mara kwa mara kama ilivyo kwa Wazir Junior.

RALLY BWALYA

Yanga walikuwa tayari wameshaanza mazungumzo na wakiamini kabla ya msimu huu kuanza watakuwa wamemsajili kiungo huyo kutokea Power Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia lakini kilicho watokeo wapinzani wao Simba wakamalizana na nyota huyo juu kwa juu.

Simba walimsajili Bwalya kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Dola za Kimarekani 50,000 ambayo kwa pesa ya hapa nyumbani ni zaidi ya Sh100 milioni. Bwalya aliyeanza kuonyesha makali yake katika tamasha la Simba (Simba Day), akipiga pasi tamu ya mwisho iliyokwenda kuzaa bao la Morrison ni moja ya wachezaji ambao wamevuta mkwanja mrefu katika usajili wa dirisha kubwa.

CARLOS CARLINHOS

Baada ya Yanga kumkosa Bwalya walitua nchini Angola kumchukua Carlinhos ambaye mwanzo wa msimu alikuwa moja ya mchezaji kipenzi kwa mashabiki wa Yanga ambao walikaa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kwa wingi katika siku mbili tofauti kumsubiri akiwasili.

Uongozi wa Yanga baada ya kumleta nchini Carlinhos walimsaini kwa mkataba wa miaka miwili usiokuwa na thamani ya zaidi ya Sh70 milioni ili kuwatumikia Wananchi ambao walitokea kumpenda kabla ya kumuona akicheza hata mechi ya kirafiki.

CHRIS MUGALU

Kutokana bado alikuwa na mkataba na timu yake ya Lusaka Dynamos ambayo inashiriki Ligi Kuu ya nchini Zambia lakini maelewano mazuri ya viongozi wa juu, Simba walitakiwa kulipa Dola 70 zaidi ya Sh140 milioni kwa pesa ya Kitanzania ili kunasa saini ya straika huyo.

Kutokana na Simba walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu wala hawakutaka kulaza damu walitoa kiasi hiko cha pesa na walikamilisha dili la Mkongomani huyo ambaye anauwezo mkubwa wa kucheza na nyavu katika nafasi chache za kufunga ambazo anapata pindi anapokuwa uwanjani.

PRINCE DUBE

Ana mabao sita na ndio kinara wa mabao katika kikosi cha Azam, usajili wake wala haukuwa na maneno mengi au kufatiliwa na mashabiki wengi wa soka hapa nchini lakini moto wake aliokuwa akionyesha uwanjani kabla ya kuumia ni jambo ambalo lilikuwa likifuatilia na wapenzi wengi wa soka. Kitita cha pesa ambacho amevuta kutoka katika kikosi hiko katika usajili wake si chini ya Sh70 milioni.

TUISILA / MUKOKO

Wakongomani wawili wa Yanga, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe walisajiliwa na kikosi hiko kutokea AS Vita inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini kwao.

Nyota hao wawili waliosajiliwa katika dirisha kubwa la usajili kwa kuwa walitoka katika kikosi kimoja usajili wao ulikuwa Dola za Kimarekani 130,000 ambayo kwa pesa ya kibongo inakuwa zaidi ya Sh300 milioni. Ukiachana na pesa hiyo ya usajili ambayo ni mkwanja mrefu ambao nyota hao walivuta wamekuwa wakichukua posho mara kwa mara kutokana na matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata katika kikosi cha Yanga msimu huu.

Uongozi wa Yanga kabla ya msimu kuanza uliweka hadharani watakuwa wakitoa posho kwa wachezaji wao kama watashinda michezo mitatu mfululizo huku wachezaji ambao watacheza watakuwa wanapata nyingi kuliko wale ambao watakuwa nje.