Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa hawa Simba, Yanga, Azam suala la muda

KUNA timu zinakimbizana kuzipata saini za  mastaa waliotemwa na wanaotajwa kuachwa Simba na Yanga, kabla ya kufungwa kwa usajili wa dirisha Jumatatu Januari 15 saa 5:59 usiku.

Tayari baadhi yao wanatajwa wanaweza wakasaini muda wowote kuanzia sasa na wengine hawajafanya maamuzi wapi wanataka kwenda kufanya


DENIS NKANE - YANGA
Winga wa Yanga, Denis Nkane kuna asilimia kubwa anaweza akajiunga na Dodoma Jiji kwa mkopo, imeelezwa kocha Francis Baraza aliyewahi kumfundisha Biashara United ndiye anataka asainiwe.


Kwa upande wa Nkane alipoulizwa juu ya tetesi hizo, alisema "Mimi mwenyewe nasikia ila sijui chochote, ninachofahamu mimi ni mchezaji wa Yanga hadi 2025."

NADO, LYANGA - AZAM
Wachezaji wa Azam Iddy Nado na Ayub Lyanga wanatajwa kutafutiwa timu kwa mkopo, kati ya timu zilizotajwa ni Singida Fountain Gate na Namungo.
 
Msimu uliopita Nado alikuwa na mabao saba, msimu huu ana mabao matatu, wakati Lyanga akiwa na bao moja (2023/24).


JOHN BOCCO - SIMBA
Siyo mara ya kwanza jina la nahodha wa Simba, John Bocco kutajwa kuachwa na klabu hiyo, awamu hii pia kuna tetesi za kutaka kulikata jina lake, ambapo timu zinazotajwa kumhitaji ni Ihefu na Singida Fountain Gate.


JESUS MOLOKO - YANGA
Jina lake linatajwa kwa kasi ndani ya Yanga kuwa kati ya wachezaji wanaoweza kutemwa na timu inayotajwa anaweza akatolewa kwa mkopo na Singida Big Stars.


JIMYSON MWANUKE-SIMBA
Ni kati ya waliondolewa kambini Zanzibar, ambako Simba jana ilicheza fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege, imeelezwa kama mambo yakienda sawa anaweza akamalizana na Mtibwa Sugar wakati wowote kuanzia sasa.

Ingawa alipotafutwa alijibu "Mimi nipo Zanzibar nasubiri fainali kati ya timu yangu Simba na Mlandege."