Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa yaitaka nafasi ya Tabora United

MASHUJAA Pict

Muktasari:

  • Mashujaa kwa sasa inashika nafasi ya nane katika msimamo kwa pointi 33 baada ya mechi 28 ambapo imeshinda nane, sare tisa na kupoteza 11, huku ikifunga mabao 28 na kufungwa 32.

UONGOZI wa Mashujaa ya Kigoma umefunguka kuwa mikakati iliyopo kwa sasa ni kushinda mechi mbili za mwisho zilizosalia ili kumaliza katika nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu Bara iliyosaliwa mechi za raundi mbili kwa sasa kabla ya kufikia tamati Juni 22.

Mashujaa kwa sasa inashika nafasi ya nane katika msimamo kwa pointi 33 baada ya mechi 28 ambapo imeshinda nane, sare tisa na kupoteza 11, huku ikifunga mabao 28 na kufungwa 32.

Ikisaliwa na mechi mbili dhidi ya KMC na JKT Tanzania zote nyumbani, ikishinda zote itafikisha pointi 39 wakati huo itategemea na matokeo ya Tabora United, JKT Tanzania na Dodoma Jiji kama timu hizo zitapoteza mechi zao zilizosalia ili Mashujaa imalize ya tano.

Hata hivyo, kama Tabora itashinda mechi moja huku JKT Tanzania na Dodoma Jiji zikafanya vibaya basi Mashujaa itamaliza katika nafasi ya sita na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Edward Swai aliliambia Mwanaspoti kuwa kwa sasa vijana hao wanaendelea na mazoezi kuhakikisha wanashinda mechi hizo mbili na kutimiza malengo waliyojiwekea.

“Tulikuwa na mapumziko mafupi ya siku 10 lakini kama wiki mbili zilizopita vijana wamerejea kambini na mazoezi ya kutafuta nafasi tano za juu yameanza,” alisema Swai.

Aliongeza, msimu huu malengo yao yalikuwa ni kumaliza katika nafasi ya tano au sita, hivyo bado wapo kwenye njia nzuri ya kufikia hizo nafasi kama watafanya vyema katika mechi mbili zilizosalia nyumbani.

“Sio kwamba mwalimu Abdallah Baresi alikuwa mbaya ndio maana tulimtoa, ni mabadiliko tu ndani ya timu yalifanyika lakini ni miongoni mwa makocha ambao wameipa heshima timu yetu,” aliongeza Swai.

Akizungumzia Ligi amesema ni ngumu kutokana na ushindani uliopo, kila timu imesajili vizuri ndio maana hata nafasi ya kuwania ubingwa imekuwa na ushindani lakini pia timu nyingi zinapambana zisicheze mtoano (play-off) kwa kukwepa kushuka daraja.