Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki wasusia Derby

Mashabiki wasusia Derby

LICHA ya Mechi kuhamishiwa uwanja wa taifa na viingilio kutolewa, bado mashabiki hawajajitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara kati ya Simba Queens na Yanga Princess.

Mchezo huo ambao umeanza saa 10:00 kwenye uwanja wa taifa umehudhuriwa na mashabiki wachache ambao hata nusu ya uwanja hawafiki.

Hata hivyo, mashabiki hao wachache waliohidhuria wamekuwa na wakihanikiza kwa nguvu zote tangu mchezo umeanza.

Vilevile timu zote zimeonekana kuanza kwa kasi ya hali ya juu na katika dakika ya saba tu Simba Queens  tayari ilishajiandikia bao la kuongoza kupitia kwa nyota wake wa Kimataifa kutoka Burundi Asha Djafari.

Yanga Princess inahitaji sana kushinda mechi hiyo ili kuondoa uteja wa kutoshinda mechi yoyote dhidi ya Simba tangu ianze kucheza Ligi Kuu msimu wa 2018-19.