Mashabiki USM Alger wajaza uwanja saa tatu kabla ya fainali CAFCC

Muktasari:
- Yanga ina dakika 90 za kupindua meza dhidi ya USM Algers na kuishtua Afrika kwa kuandika rekodi mpya.
Mashabiki wa USM Alger wajaza uwanja wa Stude du 5 Juillet wenye uwezo wa kubeba mashabiki 62,000, uwanja umeja saa tatu kablya ya fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga itakyopigwa saa 4:00 kwa saa za Afrika Mashariki.
Yanga ina dakika 90 za kupindua meza dhidi ya USM Algers na kuishtua Afrika kwa kuandika rekodi mpya.
Fainali ya kwanza Kombe la Shirikisho iliyopigwa katika uwanja wa mkapa Yanga alipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger ili Yanga achukue ubingwa CAFCC anahitaji kushinda mabao 2-0 au 3-1.
Hakuna maswali kuwa Yanga wana kazi moja tu ya kufanya ili kuweka historia nyingine ya soka hapa nchini.
Tayari vitabu vinasema kuwa Yanga ndiyo timu pekee ya Tanzania kufika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na kupoteza mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Mkapa.