Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki USM Alger waifanyia Yanga vurugu

Muktasari:

  • Mashabiki wa USM Alger usiku wa kuamkia Leo wamevamia hoteli ya Legacy ambayo kikosi cha Yanga kimeweka Kambi na kuanza kuimba nyimbo zao kwa dakika 16.

Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya Yanga kushuka Uwanjani leo  June 3 kumalizana na wenyeji wao USM Alger kundi kubwa la mashabiki wa Waarabu hao wamevamia hoteli ya Yanga na kufanya vurugu.

MACHAFUKO kutoka ALGERIA!!! YANGA yavamiwa na Mashabiki wa USM ALGER kambini ni Vurugu mwanzo mwisho

Mashabiki wa USM Alger usiku wa kuamkia Leo wamevamia hoteli ya Legacy ambayo kikosi cha Yanga kimeweka Kambi na kuanza kuimba nyimbo zao kwa dakika 16.

Hawakuishia kuimba peke yake mashabiki hao kabla ya kuondoka walipiga fataki za kutosha mbele ya hoteli hiyo  kabla ya baadaye kutawanywa na walinzi wa hoteli hiyo.

Tayari uongozi wa Yanga umesharipoti matukio hayo kwa maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wakiambatanisha na picha za video za matukio hayo.

"Tumeshawasiliana na watu wa CAF kuwapa hizi taarifa,kikosi kipo salama tulihakikisha hizi vurugu zao haziwaathiri wachezaji ingawa baadhi waliamka,"amesema bosi mmoja wa juu wa Yanga

Yanga itashuka uwanja wa ugenini Leo ikihitajj ushindi wa kuanzia mabao 2-0 dhidi ya USM Alger katika Fainali ya mkondo wa pili baada ya timu kupoteza nyumbani kwa mabao 2-1  hapa jijini Dar es Salaam.