Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Simba, Yanga tambo kibao

Muktasari:

  • Mratibu wa Yanga Mkoa wa Mwanza, Kija Malingwi alisema pamoja na wanachama na mashabiki wa timu hiyo kushiriki shughuli za kijamii kwa kufanya usafi, kutoa misaada na kuchangia damu hospitali ya Sekouture, Bugando na gereza la Butimba, wataondoka kesho kwenda jijini Dar es Salaam.

WIKENDI hii Simba na Yanga zinahitimisha kilele cha matamasha yao ya Simba Day na Wiki ya Mwananchi, huku mashabiki wa timu hizo mkoani Mwanza wakitambiana kufunika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mratibu wa Yanga Mkoa wa Mwanza, Kija Malingwi alisema pamoja na wanachama na mashabiki wa timu hiyo kushiriki shughuli za kijamii kwa kufanya usafi, kutoa misaada na kuchangia damu hospitali ya Sekouture, Bugando na gereza la Butimba, wataondoka kesho kwenda jijini Dar es Salaam.

“Leo (Ijumaa) tutasoma dua kuiombea timu yetu katika bwalo la Mgambo, nawaomba watu wahudhurie kwa wingi kwenye tamasha letu na wanachama wahakikishe wanalipia ada zao ili kuwaunga mkono viongozi wanaopambana kuifanya klabu yetu kuwa bora,” alisema Malingwi.

Shabiki wa timu hiyo, Machuma Lugwisha, alisema “Matarajio yetu siku yetu itafana kwa sababu ya tulivyojiandaa, mipango na jinsi timu ilivyocheza mechi za kirafiki tumesajili vizuri, kwa hiyo wiki ya Mwanananchi itapendeza.”

Mwanachama wa Yanga tawi la Yanga Dhahabu Geita, Deogratias Steven ‘Deototo’, alisema; “Kutokana na uongozi ulivyojipanga kila sehemu, naamini mambo yatanoga na kupendeza, nina imani kuna maingizo ambayo hayajatangazwa huenda yakawa suprize.”

Kwa upande wake, Mratibu wa Simba Mkoa wa Mwanza, Nasibu Naimocha alisema msafara wa mashabiki uliondoka jana jijini Mwanza kwenda Dar es Salaam wakiwa na matarajio makubwa ya timu yao kufanya vizuri huku usajili waliofanya ukitarajia kuongeza mzuka zaidi.

“Maboresho yaliyofanyika ni makubwa na maandalizi yameonyesha benchi la ufundi liko vizuri, basi wana Simba tuwe na imani, tujitokeze kwa wingi kuujaza uwanja tuipe morali timu na kupongeza kazi kubwa iliyofanywa na uongozi kuhakikisha timu yetu inakuwa bora,” alisemas Naimocha

Shabiki wa timu hiyo, Petro Bernard, alisema “Watani wetu tunawapelekea salamu, sisi ni next level kwa maana tumekuwa tukianza wao wanafuatia, wanabaki kuiga kila siku kwetu. Hawawezi kututisha na Chama (Clatous) ambaye tumemuacha, usajili wetu umetisha tumesafisha wazee.”