Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masaka kukaa benchi Brighton, tatizo ni hili

MASAKA Pict

Muktasari:

  • Masaka alikuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili akiuguza jeraha la bega alilopata Novemba 09 mwaka jana kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake England dhidi ya Arsenal.

MECHI mbili za mwisho ilizocheza Brighton baada ya mshambuliaji wa Kitanzania, Aisha Masaka kutoka kwenye majeraha ameendelea kusalia kwenye benchi.

Masaka alikuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili akiuguza jeraha la bega alilopata Novemba 09 mwaka jana kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake England dhidi ya Arsenal.

Jeraha hilo lilimuweka nje kwa muda huo na mwanzoni mwa mwezi Machi nyota huyo wa zamani wa Yanga Princess aliripotiwa kuanza mazoezi ya uwanjani.

Machi 16 Chama la Mtanzania huyo lilicheza dhidi ya

Tottenham Hotspurs ikishinda bao 1-0 kisha Machi 23 kupoteza na Leicester City kwa jumla ya mabao 3-2 na zote Masaka kaanzia benchi.

Tangu Masaka ajiunge na timu hiyo msimu huu akitokea BK Hacken ya Sweden, amecheza mechi mbili kwa dakika 14 dhidi ya Arsenal (4) na Birmingham (10).

Kabla ya kuitumikia timu hiyo Masaka amecheza klabu kadhaa, Hacken akicheza kwa misimu miwili na alicheza mechi 14 za mashindano yote akifunga mabao matano.

Akiwa Yanga Princess msimu wa 2020/21 aliibuka na tuzo ya mfungaji bora akiweka kambani mabao 35 na kuweka rekodi ya mzawa aliyefunga mabao mengi ambayo hayajafikiwa na mchezaji yeyote.