Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mangungu: Tufanye kampeni za hoja

Mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amewataka wagombea kufanya kampeni na kujenga hoja pasipo kuanzisha vurugu.

Mangungu ambaye anatetea kiti chake katika uchaguzi ujao unaotarajia kufanyika Januari 29 mwaka huu amesema hakuna uongozi unaofanya mabaya pekee pasipo mazuri.

Mangungu kabla hajaanza kuzungumza na wanachama aliomba kutoka ukumbini ili mpinzani wake Moses Kaluwa aanze yeye kuzungumza lakini aliambiwa kuwa ameondoka.

"Naweza nisiwe mimi na akawa mwingine lakini tufanye kampeni kwa hoja, hakuna uongozi ambao una mabaya tu kwanini wengine wanashikilia mabaya pekee.

"Tumefanya mambo mengi mazuri ndani ya Simba ila uamuzi wa kuchagua nani aongoze klabu upo mikononi mwa wanachama ambao ndio wamepiga kura," amesema na kuongeza

"Tatizo watu wanashikiria tu kwanini hatuifungi timu moja ambayo ipo hapo kwenye Mbu, mbona tumezifunga timu kubwa na tajiri Afrika hamzungumzi, mpira wa sasa ni sayansi na teknolojia."

Katika uongozi wetu ndio umeweza kuvunja hata mkataba wa Robertinho, hapa tukisema tuchangishane hata pesa ya Chama hatuwezi, lakini yanayofanywa sasa hayaonekani," amesema Mangungu