Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mandoga apeleka Mlungambunga Kenya

Muktasari:

  • Mandonga alisema pambano hilo la kukata na shoka ambalo litarushwa mubashara, litakuwa la kukata ngebe za mpinzani wake na mabondia wengine wote Afrika Mashariki kwani safari hii ana ngumi iitwayo ‘Mlungambunga’.

KARIM Mandonga 'Mtu Kazi' ametangaza kiama kwa bondia maarufu nchini Uganda, Kenneth Lukyamuzi atakayepambana naye Machi 25 kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi, Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mandonga alisema pambano hilo la kukata na shoka ambalo litarushwa mubashara, litakuwa la kukata ngebe za mpinzani wake na mabondia wengine wote Afrika Mashariki kwani safari hii ana ngumi iitwayo ‘Mlungambunga’.

"Waafrika wote wajiandae kushuhudia mtu akisulubiwa ulingoni siku hiyo mubashara ndani ya runinga," alisema Mandonga huku akisisitiza watamchapa mpinzani wake mapema sana kwa ‘knock out’.

"Nimefurahi sana kwa kukubaliwa pambano hili kuonyeshwa mubashara kwenye runinga, hii italifanya lionekane kote Afrika. Huu ni wakati wa kuionyesha Afrika na dunia kuwa Mandonga ni mtu kazi kwelikweli. Naenda kutuma salamu. Kama kuna bondia yeyote anayejiamini aje mimi kazi yangu ni moja tu – kumchapa!" Alijigamba Mandonga.

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, alisema;

"Tumeliweka pambano hili kuwapa watanzania wengi fursa ya kumuona bondia wao maarufu akiipeperusha bendera ya Tanzania kwenye ulingo wa ndondi. Huu ni mwanzo tu, tutaendelea kuhakikisha kuwa tunaongeza burudani ndani ya chaneli zetu huku tukiwapa jukwaa wanamichezo wwetu kuonekana kimataifa," alisema Shelukindo.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Mandonga alipata umaarufu mkubwa sana nchini Kenya baada ya kumtwanga bondis wa Kenya William Wanyonyi. Pambano hili kwa mara nyingine tena linatarajiwa kuwa gumzo jijini Nairobi linapofanyika ana nchini anapotoka bondia Ewano ambaye ndiye mpinzani wa Mandonga katika pambano hilo.

Kabla ya pambano hilo , bondia  Nik Otieno wa Kenya atapambana na Hassan Ndongo wa Tanzania wakati George Bonabucha  wa Tanzania atazichapa na  Michael Diares wa Afrika Kusini na mwanandoni wa kike Fatuma Yazidu ataonyeshana kazi na bondia wa Uganda,

Consolata Musanga. Pia katika pambano hilo, bondia  Zawadi Kutaka  wa Tanzania atazichapa na bondia wa Kenya, Plaxedus Odwor.