Manara awapiga dongo Yanga

Friday February 19 2021
New Content Item (1)
By Thomas Ng'itu
By Ramadhan Elias

MKUU wa Kitengo cha Habari Simba, Haji Manara ni kama vile ameipiga dongo Yanga baada ya kusema klabu kubwa ikiwa inawalalamikia marefa wanakosea.

Maneno ya Manara yanakuja muda mchache baada ya Uongozi wa Yanga kuzungumza na Waandishi wa Habari wakiwalalamikia waamuzi namna ambavyo wanachezesha mechi zao.

Akizingumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa, Februari 19, Manara amesema ni kitu cha kushangaza kwa timu kubwa kulalamikia waamuzi hadharani.

"Simba huko tumeshatoka hatuwezi kukaa tukianza kuwalalamikia waamuzi, yaani nyie mnakosa magoli ya wazi wenyewe halafu mnawalalamikia waamuzi, Mbeya City wafungeni tano halafu muone hao waamuzi watafanya nini," amesema Manara.

Manara ameongeza kwa kusema kuwa, "Halafu wewe kaka yangu kila siku unapelekwa kuongea mambo mabaya, mbona haupelekwi kwenye kutambulisha wachezaji inabidi ushtuke kwa kweli".

"Mdogo wako nikija hapa naongea tu mambo mazuri zuri, ukinipa mambo mabaya walaa siyataki,".

Advertisement

Manara amefunguka zaidi na kusema muda mwingine Yanga wakiona Benard Morrison anafunga basi wanaita mikutano.

"Basi Morrison atakuwa hachezi tena maana akifunga tu ujue wataita mikutano, haya watacheza wakina Meddie Kagere ili wafunge wao".

Advertisement