Buku tatu tu kuwaona Simba, Al Ahly

Friday February 19 2021
New Content Item (1)
By Thomas Ng'itu
By Ramadhan Elias

MABOSI wa Simba wameona pesa sio ishu kubwa kwao zaidi ya ushindi, kwani wamewawekea viingiilio vidogo mashabiki wao ili kuhakikisha mashabiki wanaingia kwa wingi kuisapoti timu yao.

Kiingilio cha chini kabisa katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly ya Misri ni Sh 3000 kwa mzunguko ambapo mechi hiyo itachezwa wiki ijayo Jumanne ya Februari 23, uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano cha Simba, Haji Manara amesema kuwa; "Kiingilio hiki kama kweli wewe ni mwanasimba basi hauwezi kukaa nyumbani zaidi utakuja uwanjani kuisapoti timu yako".

Manara amesema tiketi za mchezo huo zinaanza kuuzwa leo Ijumaa na ikifika Jumatatu usiku basi wanaweza kupandisha bei.

"Ni bora watu waanze kununua tiketi leo kwani vituo vimefunguliwa, hakuna haja ya kubanana tena milangoni."

Upande wa bei zingine ni Sh 15000 kwa  VIP B na VIP A ni Sh 30000.

Advertisement
Advertisement