Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabondia wafunguka; Mayweather vs McGregor

ALFAJIRI ya Jumapili hii litapigwa pambano la masumbwi linalotajwa kuwa ni la karne wakati bondia Floyd Mayweather ambaye kambi yake inajulikana kwa jina la Money Team atakapozipiga na Conor McGreagor, lakini mabondia wengine maarufu wamesema Money Team itashinda mapema tu.

Bondia mashuhuri, Mike Tyson amesema Conor hana mbinu za kupigana na Floyd na ndiyo maana anaona atapigwa asubuhi tu, sawa na ilivyo kwa mtazamo wa mabondia wengine akiwamo Anthony Joshua.

Tyson alisema: “Conor hana ujuzi wa kutosha kucheza ngumi n Floyd. Kama anapigana kule kwenye ngumi za vizimba siyo kwenye masumbwi haya, labda kama ataruhusiwa kurusha mateke.”

Anthony Joshua alisema: “Utakuwa ushindi mwepesi sana. Cheki mabondia ambao Mayweather amewachapa, walikuwa mabondia mahiri, lakini kwa Floyd walionekana wa kawaida tu. Hao mabondia aliowapiga Mayweather, Conor hawawezi.”

Bondia Ricky Hatton naye alizungumzia pambano hilo akisema: “Mimi ni shabiki wa Conor McGregor, lakini kuhusu mapambano lake ni kitu tofauti.

“Mimi nilipigana na Mayweather sikumpiga, Oscar De La Hoya hakumpiga, Canolo Alvarez hakumpiga, hivyo hata Conor hawezi kumpiga.”

Evander Holyfied alisema: “Labda tu kama atamfanyia rafu ndani ya ulingo kumtibua akili yake, pengine hilo ndilo litakaloweza kumsaidia.”

Pambano hilo limekuwa maarufu zaidi kwa siku za karibuni na kwamba ubishi wa nani mbabe utafika tamati alfajiri ya Jumapili kwa saa za Afrika Mashariki.