Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabeki Yanga watuma salama kwa mashabiki

Oscar Joshua

Muktasari:

Wikiendi iliyopita, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa, ilimwidhinisha Okwi kucheza Simba baada ya Yanga kukiuka masharti ya mkataba dhidi ya mchezaji huyo.

BEKI wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua, amewaambia mashabiki wa Yanga wasibabaishwe na kuondoka kwa straika Emmanuel Okwi kwenda Simba kwani watamshugulikia ipasavyo uwanjani hata wakikutana naye kwenye mechi leo Alhamisi.

Wikiendi iliyopita, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa, ilimwidhinisha Okwi kucheza Simba baada ya Yanga kukiuka masharti ya mkataba dhidi ya mchezaji huyo.

Joshua ambaye anasifika kwa kucheza kwa nguvu, amesisitiza kwamba Okwi hakatizi ataishia kutamba tu nje ya uwanja.

“Okwi namjua hata kabla hajajiunga na Yanga, nafahamu anavyocheza na nimejiandaa kumzuia hata kama tutacheza kesho (leo). Ni mchezaji mzuri lakini siyo anayetisha kivile katika kumzuia,” alisema Joshua.

“Mashabiki wanamchukulia Okwi kama mtu maalumu lakini si kweli kwani hawezi kufanya kila kitu peke yake, sisi tutamdhibiti.”

Beki huyo mwenye taaluma ya Uandishi wa Habari, amesisitiza kwamba yeye na wenzake wamejipanga kikamilifu kukabiliana na straika yeyote yule na huwa wanazungumza mara kwa mara ndani na nje ya uwanja kuhakikisha wanakuwa na lengo moja timu ishinde.

Uhakika wa Okwi kukutana na Joshua ni Oktoba 12 katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayozikutanisha Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Okwi aliichezea Yanga kuanzia Desemba mwaka jana hadi Machi mwaka huu baada ya hapo akawa katika mgogoro wa malipo na uongozi wa timu hiyo mpaka alipojiunga na Simba mwishoni mwa mwezi uliopita. Joshua ambaye ni beki mahiri wa Taifa Stars, amecheza mechi nyingi za Simba na Yanga na amekuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji.