Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yazipiga bao Yanga, Simba

AZAM Pict


LICHA ya Azam kumaliza msimu wa 2025-2026 katika Ligi Kuu ya NBC ikiwa nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 64, nyuma ya Simba iliyomaliza nafasi ya pili na pointi 73 na mabingwa Yanga waliokusanya pointi 75, lakini imewapiga bao wakongwe hao kwa namna nyingine.


Azam imeweka rekodi ya kipekee katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025-2026 ya kucheza mechi zote 15 za nyumbani bila ya kuruhusu bao, ikizipiga bao timu zote ikiwemo Simba na Yanga.


Katika mechi 15 ilizocheza Azam msimu huu nyumbani za Ligi Kuu, imeshinda 11 na sare nne, ambapo kikosi hicho kimefunga mabao 25, nyavu zake hazijatikiswa.

AZA 03

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya tano mfululizo na mara 32 kijumla, mechi 15 za nyumbani imeshinda 14 na kutoka sare moja, huku ikifunga mabao 49 na kuruhusu matatu.

Kwa upande wa Simba iliyomaliza nafasi ya pili, katika mechi 15 za nyumbani, imeshinda 12, sare mbili na kupoteza moja, huku ikifunga mabao 30 na kuruhusu sita.

AZA 02

Licha ya Azam kuzishinda Yanga na Simba kwa kucheza mechi 15 za nyumbani za Ligi Kuu kwa msimu wa 2025-2026 bila ya kuruhusu bao, lakini hakuna timu nyingine iliyofanya hivyo, ikiwa ni rekodi ya kuvutia kwa kikosi hicho.

Akizungumzia hilo, Kocha wa Azam, Mkongomani Florent Ibenge amesema sio jambo rahisi kutokana na ushindani ulivyokuwa mkubwa kutoka kwa wapinzani wao, ingawa hali hiyo inaonyesha jinsi wachezaji wanavyojua thamani ya uwanja wa nyumbani.

AZA 01

“Kwetu ni jambo nzuri kwa sababu inaonyesha tunaweza kufanya zaidi ya hicho tulichokifanya, mwenendo huu tungekuwa nao pia kwa mechi za ugenini nadhani tungesema mengine, japo nikiri ni motisha zaidi kwetu kwa msimu ujao,” amesema Ibenge.

Kwa ugenini, Azam imeruhusu mabao 12, huku ikifunga 21 katika mechi 15 ambapo imeshinda saba, sare sita na kupoteza mbili.

Timu iliyoruhusu mabao mengi nyumbani ni Fountain Gate ambayo ni 24, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar (23), kisha KMC (22).

Mashujaa yenyewe imefunga mabao tisa nyumbani na kuruhusu tisa, ikiwa ni timu ya nne kwa kuruhusu mabao machache nyumbani.

Katika hatua nyingine, Azam na Yanga ndiyo timu pekee ambazo hazijapoteza nyumbani, huku rekodi hiyo ugenini inashikiliwa na Simba ikiwa ndiyo pekee haijapoteza.