Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Shinyanga inaanza upyaaa

SHINYANGA Pict

Muktasari:

  • Kamishna wa ufundi  na mashindano  wa Ligi hiyo George Simba, amesema Ligi ya mkoa huo  ilisimama kupisha mashindano ya Kombe la Taifa.

LIGI ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Shinyanga inatarajia kuendelea Jumapili, kwa mchezo kati ya timu ya B4 Mwadui na Risasi.

Mchezo huo wa Ligi ya Mkoa, utafanyika kwenye Uwanja wa Risasi.

Kamishna wa ufundi  na mashindano  wa Ligi hiyo George Simba, amesema Ligi ya mkoa huo  ilisimama kupisha mashindano ya Kombe la Taifa.

Alisema Ligi itaendelea tena kesho (Jumatatu)  kwenye Uwanja wa Kahama   kwa mchezo kati ya timu ya Kahama Six-ers na Veta.

Simba alisema bingwa mtetezi wa Ligi hiyo Kahama Sixers anaongoza kwa pointi 6, akifuatiwa na Risasi yenye pointi 4.

 Alitaja timu zinazoshiriki mwaka huu  ni B4 Mwadui, Risasi, Kahama Sixers na Veta.

Kwa mujibu wa Simba, mfumo utakaotumika, ni wa kila timu kucheza nyumbani na ugenini.

Alisema timu itakayoshika nafasi ya kwanza itacheza na ya nne, ya pili na ya tatu, na kila timu itacheza michezo mitatu “best of three playoffs”.