Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu Zanzibar vitani tena Oktoba 5

MZUNGUKO wa tano wa Ligi Kuu Soka Zanzibar (PBZ PL), keshokutwa Oktoba 5 unatarajiwa kuanza kwa mechi mbili moja itapigwa kwenye Uwannja wa Mao Zedong A, na nyingine kwenye Uwanja wa Finya.

Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Chipukizi, timu ya KMKM watashuka dimbani kucheza dhidi ya Ngome FC Mao Zedong na Chipukizi watacheza na Maendeleo huko Finya mechi zote zitachezwa saa 10:15 jioni.

Mpaka muda huu ikiwa timu zote zimeshacheza mechi nne Kuna baadhi ya timu hazijafanikiwa kupata ushindi hata mechi moja na hivyo kuwafanya mashabiki wao kukosa raha.

Timu za Mafunzo, Jamhuri, Hard Rock, Ngome FC na New City hizi hazijaonja ladha ya ushindi tangu kuanza kwa ligi msimu huu NA zimekuwa na wakati mgumu jambo ambalo huenda likapelekea kuwapoteza mashabiki wao.

Msemaji wa klabu ya Ngome Fatawi Ramadhan, anasema hawaridhishi na mwenendo wa timu yao kwani mambo yamekuwa tofauti na walivyotarajia.

Alisema katika mechi walizocheza tayari wapo nje ya malengo kwani kuna baadhi ya mechi walikuwa wamezipa asilimia kubwa ya kushinda hatimaye wameangukia pua na bado kuna ugumu wa kupata alama tatu maana mchezo unaofuata wanakwenda kukutana na mpinzani mgumu KMKM.

New City FC timu ambayo ilipanda ligi kuu kwa kishindo na kuwa na matarajio makubwa lakini mambo yamekuwa tofauti na wao hawajashinda mechi hata moja mpasa sasa.

Walianza ligi wakiwa na mashabiki wengi nyuma yao lakini kadri wanavyofanya vibaya wanazidi kuwapoteza mashabiki wao maana watu wanataka ushindi na  hilo limekuwa gumu kwao.

Je! Timu hizo zitakwenda kutoboa kwenye mzunguko wa tano ili mashabiki wao wawe na furaha kama ilivokuwa kwa mashabiki wa timu za KVZ, na JKU?