Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lema amtaja Raphael Daud

Lema amtaja Raphael Daud

MTANZANIA Michael Lema anayecheza soka la kulipwa Austria kwenye klabu ya TSV Hartberg, amesikitishwa na kupotea kwa aliyekuwa kiungo wa Mbeya City na Yanga, Raphael Daud.

Lema alisema jina la Raphael Daud bado lipo kichwani mwake maana ni mchezaji ambaye alikuwa akiamini kuwa anaweza kucheza soka la kulipwa Ulaya.

“Alikuwa akifanya vizuri Yanga lakini mara alizimika kama mshumaa, sijui ni shida gani iliyotokea kwake, nadhani alitakiwa kujengwa na sio kuonyeshewa malango wa kutokea, kwa huku Ulaya mchezaji amekuwa akitazamwa kwa ukaribu sana,”

“Kuna muda unaweza kushindwa kucheza kwa kiwango chako kumbe kuna mambo ambayo yanakutatiza, wanasaikolijia watakaa na wewe chini kwa ajili ya kukusaidia na mwisho wa siku unarejea kwenye mstari,” alisema winga huyo mwenye kipaji.