Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwani Popadic alikuwa mwalimu mashuleni

Muktasari:

Kumpiga mtu ni kosa kisheria, hata kama si kisheria ila sio busara na si haki ya mtu kwani kuna njia nyingi za kumwadhibu mchezaji ambaye anaonekana ana utovu wa nidhamu ama vinginevyo.

Dar es Salaam.Uongozi wa Singida United umemtimua kocha wao Dragan Popadic raia wa Serbia ikitajwa sababu moja kubwa kwamba alikuwa anawakalipia sana wachezaji wake pamoja na kuwapiga.
Kauli hiyo ilitolewa na mmoja wa Wakurugenzi wa klabu, Festo Sanga mapema wiki hii ingawa wadau wengi wa soka walionekana kutoiamini kauli ya Sanga juu ya maelezo ya kumtimua kocha wao ambaye alichukuwa nafasi ya Hans Pluijm .
Popadic hajadumu sana na kikosi hicho ambapo alisaini mkataba wa miezi sita tangu Januari 12 mwaka huu na hivi karibuni alikaririwa kuulalamikia uongozi wa timu kuwalaza wakiwa wamekula ndizi tatu tu.
Inawezekana maswali ya wadau wengi wa soka hayakujibiwa kwani huenda haijawahi kutokea kwenye ligi kuu kuona kocha akimpiga mchezaji ingawa kutukana matusi huwa inaelezwa kufanywa na baadhi ya makocha kwa wachezaji wao hasa pale wanapofanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
Mbali na hatua hiyo imekuwa kawaida kwa makocha ambao wanazingatia nidhamu kuwapa adhabu wachezaji wao ikiwemo kutompanga kikosini ama kumkata mshahara wake na si kumpiga kama inavyodaiwa kufanywa na Popadic.
Kitu kilichonistua ni pale ambapo wachezaji kudai kwamba kocha huyo ambaye aliwahi kuifundisha Simba miaka ya nyuma alikuwa nafanya vitendo hivyo, yaani ukali ulipitiliza hata kwa wenzake wa benchi la ufundi.
Alichokuwa anakifanya Popadic huenda ni kama kile wanachokifanya waalimu wa shule ya msingi ama sekondari kuwachapa wanafunzi wanapokosea ingawa siku hizi tabia za kuchapa wanafunzi nazo zimepungua kwa asilimia kubwa kwani kumchapa mtu sio kumfundisha zaidi unampa usugu.
Singida United haina mwenendo mzuri kwenye ligi, imekuwa ikikutana na changamoto nyingi za kukimbiwa na wadhamini mara wanapomaliza mikataba yao, kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji wao hadi inafikia sasa inakimbiwa na wachezaji ambao wamekosa uvumilivu wa kuishi bila mshahara.
Hili la kocha limeibuka kuwa jipya sasa ndani ya Singida na pengine viongozi wameona watumie busara tu ya kuachana naye maana huenda yangetokea maafa makubwa maana kuna wachezaji ambao uvumilivu wao ni mdogo wangeweza kumrudishia kisago kocha wao na kusababisha matatizo makubwa.
Kumpiga mtu ni kosa kisheria, hata kama si kisheria ila sio busara na si haki ya mtu kwani kuna njia nyingi za kumwadhibu mchezaji ambaye anaonekana ana utovu wa nidhamu ama vinginevyo.
Niwapongeza tu wachezaji wa Singida United hawakuchukuwa hatua ya kumjibu kwa vitendo kocha huyo kwani kungewaletea shida sana kisheria ukizingatia ni raia wa kigeni ambapo anegonekana kunyanyaswa ugenini, kukaa kimya ni busara  kubwa sana na inaepusha mambo mengi.
Pia uamuzi waliyoyafanya viongozi wa Singida United nayo ni ya busara kuliko wangemwacha aendelee kuwepo ndani ya timu pengine naye angeleta madhara makubwa zaidi kwa wachezaji ama kupelekea timu yao hata kushuka daraja kwani wachezaji wangecheza kwa uoga na wanasema uoga ukizidi unaharibu mambo.
Lakini hili litakuwa funzo kwa hizi timu kukurupuka kuajiri makocha wa kigeni bila kufuatilia vizuri historia zao za miaka ya karibuni kwani inaonekana wengi hukariri viwango vyao vya miaka ya nyuma zaidi.
Vongozi wakumbuke kwamba maisha ya binadamu hubadilika siku hadi siku, hivyo hakuna ulazima wa kumwajiri kocha ama mtu kwa kufuata historia ya miaka zaidi ya mitatu nyuma.
Ajira ziendane na mabadiliko na mahitaji ya wakati huo, huwa inashangaza, inasikitisha klabu moja kufundisha na makocha zaidi ya wawili ndani ya msimu mmoja yote haya ni kushindwa kufuatilia kwa kina tabia zao.
Mara kadhaa husikika ikisemwa kwamba kocha huyu anagawa timu, mara anapendelea ama analeta mpasuko kwenye timu anaacha lakini baada ya muda utasikia timu nyingine imempa ajira ingawa kweli wapo wanaosingiziwa kuwa na tabia hizo wakati hawana.
Singida United hilo ni funzo kwenu maana timu bado changa sana kwenye ligi lakini ina changamoto kibao.