Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Mkapa kweupeee

NDANI Pict
NDANI Pict

Muktasari:

  • Saa 11 kamili jioni itachezwa mechi ya dabi ya Kariakoo kati ya mwenyeji wa mchezo huo Yanga na Simba ambao utahitimisha msimu wa 2024/25.

UWANJA wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam ambao utatumika kuchezewa mechi ya dabi kati ya Yanga na Simba uko mweupe kwenye baadhi ya majukwaa.

Saa 11 kamili jioni itachezwa mechi ya dabi ya Kariakoo kati ya mwenyeji wa mchezo huo Yanga na Simba ambao utahitimisha msimu wa 2024/25.

Lakini zikiwa zimesalia saa chache kabla ya kupigwa mtanange huo bado mashabiki wa soka wanaendelea kuongezeka majukwaani.

Idadi kubwa inaonyesha ni jezi za njano na kijani zikitawala uwanjani hapo huku jezi nyekundu na nyeupe zikionekana baadhi ya eneo.

Hata hivyo bado mashabiki wanaendelea kuingia mmoja mmoja na sehemu nyingi zikionekana kweupe.

Pambano hilo la kufungia msimu wa Ligi Kuu 2024-2025 unapigwa muda mchache ujao kuanzia saa 11:00 jioni ambao utatangaza bingwa mpya baada ya kuahirishwa mara mbili Machi 8 na Juni 15, ikiwa ni miaka nane tangu mara ya mwisho bingwa kupatikana mechi ya mwisho msimu wa 2016-2017.