Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Simba hawaiwezi Prisons

TANZANIA Prisons imeendeleza ubabe wake kwa klabu ya Simba baada ya kushinda bao 1-0 mechi ya Ligi ya Vijana chini ya miaka 20 inayoendelea nchini.

Bao hilo limefungwa Mwaka Mwakifuna dakika za nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika wakiwa 0-0 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za Simba dhidi ya timu hiyo baada ya kutoshinda msimu uliopita na huu huku timu wakubwa inayoshiriki Ligi Kuu ilifungwa bao 1-0 kama ambavyo imejirudia leo.

Mechi ya kwanza Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC na leo mechi ya pili wamepoteza huku watani wao Yanga wakishinda mechi zote mbili ya kwanza dhidi ya Namungo Uwanja wa Majaliwa na leo uwanja wa Mkwakwani Tanga wametoka kifua mbele kwa mabao 2-1.

Mechi ijayo Simba itakuwa mkoani Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar ambayo leo imeshinda bao 1-0 dhidi ya Ihefu katika dimba la Highland Estate.

Matokeo ya mechi nyingine za leo;

Dodoma Jiji 1-1 Biashara Utd