Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kula Bata? Mbeya City sahauni

Wachezaji wa Mbeya city .

Muktasari:

Phiri aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Ilikuwa ni vigumu kuwa na kikosi kingine kwani nilikuwa na wachezaji wachache hivyo nililazimika kuwatumia wachezaji wengine hata ambao hawachezi nafasi zenye mapungufu, sasa nahitaji kuwa na kikosi kipana zaidi, kitu pekee ninachokihitaji ni kuendelea kutengeneza timu pasipo mapumziko.

        MBEYA City ilianza ligi vibaya ambapo wadau wengi walijua kwamba timu hiyo ingeshuka daraja kutokana na mwenendo mbovu lakini uongozi wa City uliamua kuajiri kocha mpya, Kinnah Phiri raia wa Malawi ambaye ameiwezessha timu hiyo kubaki kwenye ligi msimu ujao na imemaliza ikiwa nafasi ya nane.

Phiri aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Ilikuwa ni vigumu kuwa na kikosi kingine kwani nilikuwa na wachezaji wachache hivyo nililazimika kuwatumia wachezaji wengine hata ambao hawachezi nafasi zenye mapungufu, sasa nahitaji kuwa na kikosi kipana zaidi, kitu pekee ninachokihitaji ni kuendelea kutengeneza timu pasipo mapumziko.

“Kikosi kijacho hakitakuwa na wachezaji wengi wakongwe, nataka wachezaji watatu ambao hawavuki miaka 30 na wengine ni wale wenye miaka chini ya hiyo huku walio na umri wa miaka 20 ndiyo watakuwa wengi, hivyo kuanza maandalizi mapema kutasaidia timu kuwa imara zaidi, maandalizi ya mapema pia yatanisaidia kujua mapungufu ya wachezaji wapya,” alisema Phiri.

Kocha huyo alisema kuwa jana Jumatatu alitarajia kukutana na waajiri wake kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo wachezaji wanaotemwa na watakaosajiliwa ambao wataingia kambini Juni 15 nchini Malawi.

“Kwasababu tayari tulikwishapendekeza majina ya wachezaji watakaosajiliwa hivyo itakuwa rahisi kuwapata kabla ya tarehe hiyo ambapo nataka timu iende Malawi kwa ajili ya mechi za kirafiki halafu turudi hapa, kambi hiyo itahusisha pia wachezaji wapya,” alisema.