Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kramo jukwaani Kwa Mkapa

WINGA wa Simba asiyetumika kwenye mechi za timu hiyo, Aubin Kramo ametinga jukwaa la Wanahabari ili kushuhudia pambano wa kikosi hicho dhidi ya Al Ahly ya Misri linalopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa usiku huu.

Muivory Coast huyo ambaye tangu asajiliwe Simba msimu huu, hajawahi kucheza mchezo wowote wa mashindano ikiwamo Ligi Kuu Bara wala mechi za kimataifa kutokana na majeraha ya muda mrefu, japo kwa sasa yupo fiti akiendelea kujifua na wenzake.

Staa huyo aliyesajiliwa Simba msimu huu kutoka ASEC Mimosas iliyowaachia pia Pacome Zouzoua na Yao Kouassi waliopo Yanga kwa sasa, ameshuhudiwa na Mwanaspoti Kwa Mkapa akiwashuhudia wenzake akiwa na rafiki zake.


Nyota huyo huenda akamaliza msimu mzima akiendelea kuwatazama wenzake akiwa jukwaani kutokana na kuchomolewa kwenye usajili wa ndani na hivyo kumzuia pia kuitumikia Simba kimataifa licha ya kuendelea kuhudumiwa na klabu kulingana na mkataba wa miaka miwili alionao Simba.

Kukosekana kwake kikosini kumefanya nafasi aliyotumika kuzibwa na mastaa wengine akiwamo Kibu Denis, Willy Onana, Saido Ntibazonkiza, Luis Miquissone, Edwin Balua, Ladack Chasambi na Saleh  Kalabaka ambao wote wapo fiti na wanauwasha kweli kweli.