Kocha Serengeti awaibua vijana 25 Umisseta

Muktasari:
Milambo alisema kuwa katika mashindano hayo mpaka hivi sasa ameshafanikiwa kupata wachezaji 25 watakaokuwa katika timu ya Vijana chini ya miaka 16 na chini ya miaka 20 ambao atawajumuisha katika vikosi vyake.
Kocha Oscar Millambo wa Serengeti Boys amesema ameamua kwenda kuangalia vipaji katika mashindano ya Shule za Sekondari ya Umisseta kwa ajili ya timu za vijana chini ya miaka 16 na chini ya miaka ishiri mkoani Mwanza.
Milambo alisema kuwa katika mashindano hayo mpaka hivi sasa ameshafanikiwa kupata wachezaji 25 watakaokuwa katika timu ya Vijana chini ya miaka 16 na chini ya miaka 20 ambao atawajumuisha katika vikosi vyake.
“Nahitaji wigo mpana katika kutafuta wachezaji na ndio sababu ya mimi kuja katika mashindano haya kuangalia vipaji. Hii ni sehemu ambayo kunakuwa na wachezaji wengi wenye umri mdogo na vipaji vikubwa kwa hiyo nitapata vijana,” alisema.
“Ilikuwa sio kazi rahisi katika kuchagua kutokana kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo, lakini mpaka hivi sasa nimefanikiwa kupata wachezaji 25 ambao wapo chini ya miaka 16 na 20 hivyo tutakuwa nao katika vikosi vyetu vya vijana,” alisema.