Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Ken Gold: Nakwenda kujitathimini 

Kocha Pict
Kocha Pict

Muktasari:

  • Fikiri ametangaza hilo leo baada ya mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC kumalizika, huku timu yake ikiendelea kusotea ushindi wa kwanza.

Wakati Ken Gold ikipokea kipigo Cha tatu kwa kupoteza bao 1-0, kocha wa timu hiyo, Fikiri Elias anafikiria kuachia ngazi kuifundisha.

Fikiri ametangaza hilo leo baada ya mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC kumalizika, huku timu yake ikiendelea kusotea ushindi wa kwanza.

Kocha huyo aliyasema hayo wakati akihojiwa na Azam TV, mara baada ya mchezo huo kumalizika akisema ameamua kuchukua uamuzi wa kujitathimini kutokana na kuona mambo kuwa magumu ndani ya timu hiyo.

"Nimeona mambo hayaendi kama ambavyo tulikuwa tunatarajia kabla. Nimeona nichukue uamuzi huo wa kujitathimini kuendelea kuifundisha timu hii,* amesema Fikiri.

"Nachukua uamuzi huu kwa weledi kulinda taaluma yangu. Inawezekana kuna mambo ambayo yanaweza kuisaidia timu kwa hatua nitakayochukua."

Ken Gold imepoteza mechi zake tatu za kwanza ikiruhusu mabao sita huku  ikifunga mabao mawili.