Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Kagera Sugar afichua kinachowafelisha

Kagera Pict
Kagera Pict

Muktasari:

  • Kagera Sugar ambayo imecheza mechi nne msimu huu, bado inasaka angalau kufunga bao la kwanza kwani haijafanikiwa kutikisa nyavu za wapinzani hadi sasa.

KITENDO cha Kagera Sugar kushindwa kupata hata bao moja katika dakika 360 ambazo ni sawa na mechi nne za Ligi Kuu Bara, kimemfanya kocha wa timu hiyo, Paul Nkata kutaja mambo manne yaliyopo nyuma yake.

Kagera Sugar ambayo imecheza mechi nne msimu huu, bado inasaka angalau kufunga bao la kwanza kwani haijafanikiwa kutikisa nyavu za wapinzani hadi sasa.

Timu hiyo yenye maskani yake mkoani Kagera, juzi Jumatatu ilipata pointi moja ikiwa ni ya kwanza baada ya kuambulia suluhu nyumbani dhidi ya JKT Tanzania. Kabla ya hapo ilipoteza mechi tatu za awali dhidi ya Singida Black Stars, Yanga na Tabora United.

Kocha Nkata amesema anachokiona kinachosababishwa na hayo ni kuchelewa kwake kufika ndani ya timu, lakini pia vijana wake kukosa bahati ya kufunga kwani nafasi wanatengeneza.

Pia amebainisha kwamba, anaona bado kuna shida katika eneo la kiungo na ushambuliaji ambapo anaendelea kuyafanyia kazi.

“Tunatengeneza nafasi lakini tunakosa bahati ya kufunga, naamini katika mechi zijazo hili tatizo litapata suluhu ingawa ninaona bado kuna shida katika kiungo na ushambuliaji,” alisema Nkata.

“Unajua nilifika katika timu kwa kuchelewa, lakini pia mimi ni mgeni hapa, hivyo nahitaji muda kufahamu wachezaji gani wanaweza kuingia kwenye mfumo ambapo itakuwa rahisi kupata matokeo mazuri.”

Mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa juzi Jumatatu Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, ulimalizika kwa matokeo ya suluhu. Matokeo ya mechi hiyo ambayo haikuzaa bao lolote baina ya timu hizo ni mara ya kwanza kutokea tangu msimu wa 2018/19 ambapo wamekutana mara tisa sasa.