Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Dodoma Jiji apangua safu ya ulinzi dhidi ya Yanga

Muktasari:

Dodoma Jiji inacheza na Yanga ambao ndio wenyeji wa mchezo wa leo unaochezwa uwanja wa Sheikh Amr Abeid Arusha

Arusha. KOCHA Mbwana  Makata wa Dodoma Jiji, kwa mara ya kwanza leo amefanya mabadiliko ya eneo la mabeki wa kati, akipangua pacha ya mabeki Augustino Nsata na Mbwana Kibacha.

Katika kikosi cha leo ambacho kina kazi ya ziada kuhakikisha eneo lao la ulinzi linakuwa na ubora zaidi kulingana na timu wanayocheza nayo leo.

Katika michezo yote 14 iliyopita kwa Dodoma Jiji, mchezaji Augustino Nsata hajawahi kuanzia benchi, lakini katika mchezo wa leo ameanzia benchi na nafasi yake imechukuliwa na beki Justine Omary.

Hii inamaanisha kwamba, kwa mara ya kwanza leo ile pacha iliyozoeleka ya mabeki Augustino Nsata na Mbwana Kibacha, imepanguliwa kutokana na Nsata kuanzia benchi.

Kabla ya leo, Pacha hiyo iliwahi kukosekana kwenye mchezo mmoja pekee dhidi ya Polisi Tanzania, ambapo ilitokana na Mbwana Kibacha kuwa na kadi tatu za njano zilizomzuia kucheza mchezo huo uliochezwa uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Justine Omary, licha ya kuaminiwa leo, mchezo dhidi ya Yanga utakuwa wa pili kwake, akiwa na kazi ya ziada kuhakikisha anailinda safu nzima ya ulinzi akishirikiana na Kibacha ambaye ndiye nahodha wa Dodoma Jiji.

Mabeki hao wataongezewa nguvu upande wa pembeni na mabeki George Wawa upande wa kulia na kushoto anacheza Jukumu Kibanda.

Katika hatua nyingine, Kocha Makata hatimaye amemuanzisha kikosi cha kwanza nyota Dickson Ambundo ambaye alikuwa anatokea benchi kwenye mechi za hivi karibuni, atatokea upande wa pembeni pamoja na Peter Mapunda.

Katika eneo la kiungo wa kati, Salmin Hoza atacheza kiungo wa ulinzi pamoja na Steve Mganga wakati washambuliaji ni Mcha Khamis na Seif Karihe.


Na Matereka Jalilu