Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Amunike atua Arusha kuongezea nguvu Serengeti Boys

Muktasari:

Amunike ametua jijini Arusha kuja kuipa sapoti timu ya Serengeti Boys kwa ajili ya maandalizi yao ya kuelekea kwenye mashindano ya UEFA Assist yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini Uturuki.

ARUSHA.  Kocha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Emmanuel Amunike ametua jijini Arusha kuja kuipa sapoti timu ya Serengeti Boys kwa ajili ya maandalizi yao ya kuelekea kwenye mashindano ya UEFA Assist yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini Uturuki.

Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ iko jijini Arusha kwa kambi ya mda mfupi kabla ya kuelekea nchini Uturuki kwenye mashindano ya UEFA Assist waliyoalikwa na pia maandalizi ya Fainali za mataifa ya Africa kwa vijana yatakayofanyika Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Serengeti Boys inayonolewa na kocha wake mkuu Oscar Milambo, mapema leo hii asubuhi Amunike ametua katika kambi hiyo na anatarajiwa kuonekana kwenye mazoezi ya kikosi hicho katika Uwanja wa Aga Khan  kesho.

Awali, akizungumza na waandishi wa habari, juu ya sababu za kuweka kambi Arusha, alisema kuwa kutokana na hali ya hewa ya ubaridi iliyoko mkoani hapa ambayo ni sawa na ya Uturuki wanapoelekea kushiriki mashindno hayo ya UEFA Assist waliyoalikwa.

“Kwa sasa Ulaya kuna baridi sana hivyo kufanya mazoezi Dar es Salaam penye joto na hewa nyingi ya Oxygen inayosababishwa na ukaribu wa usawa wa bahari, tungewapa shida sana wachezaji wetu kwenda kufanya vizuri na kuleta ushindani huko. Hivyo tumeona ni bora waje Arusha mkoa wenye baridi kutokana na kuwa mbali na usawa wa bahari hali inayofanana na tunapoenda ili miili yao ianze kuzoea.”