Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha afunguka sababu mbili kumtema Aziz KI

Aziz Pict
Aziz Pict

Muktasari:

  • Staa huyo ambaye msimu uliopita alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 21 na kumpiku kiungo mwenzake wa zamani Yanga, Feisal Salum anayekipiga Azam FC aliyekuwa nayo 19.

WAKATI maswali yakiwa mengi kuhusu kukosekana kwa Stephane Aziz Ki katika timu ya Taifa ya Burkina Faso, Kocha wa kikosi hicho, Brama Traore ametaja sababu mbili za kutomuita.

Staa huyo ambaye msimu uliopita alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 21 na kumpiku kiungo mwenzake wa zamani Yanga, Feisal Salum anayekipiga Azam FC aliyekuwa nayo 19.

Huu ni msimu wa tatu kwa Aziz Ki ndani ya Yanga, lakini tangu uliopita wote hakukosa mechi za timu ya Taifa, huku katika ligi akiwa amecheza mechi 10 na dakika 740.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha wa Burkina Faso, Traore amesema mchezaji kama Aziz Ki kutoitwa kwake timu ya Taifa haimaanishi kiwango chake si kizuri.

Amesema ni lazima watu waelewe kwamba kuna wakati kocha anakuwa na mipango kutokana na mchezo ulio mbele yake, hivyo anajua ni mchezaji gani anamhitaji na kwa nini kwani hawezi kuwatumia wote.

"Maamuzi yangu ya kumuacha Azizi Ki yana sababu mbili. Kwanza ni kutoa nafasi kwa wachezaji wengine  ambao walikuwa hawaitwi timu ya Taifa baada ya kikosi chetu kufuzu kwenda Afcon," amesema.

"Sababu ya pili ni kutokana na kumpa muda wa kupumzika kwa kuwa alitumia nguvu kubwa msimu uliopita na pia namuona kama ana uchovu uliotokana na majukumu ya klabu yeke."

Kocha huyo ameongeza: "Bado Aziz ana nafasi kubwa ndani ya timu ya Taifa ya Burkina Faso kutokana na kipaji chake na hata umri wake unaruhusu."

Katika kundi L la kufuzu Afcon 2025, Burkina Faso ndiyo inayoongoza ikiwa na alama 10 sawa na Senegal inayoshika nafasi ya pili zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwa sasa Aziz yupo pamoja na wachezaji wenzake wa Yanga ambao hawajaitwa katika timu za taifa wakiendelea na mazoezi kujinoa kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AL Hilal ya Sudan.