Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Africain amtaja Mayele

KOCHA Mkuu wa Club Africain, Bertrand Marchand amesema moja ya staa wa Yanga anayemuhofia katika mchezo wa kesho wa mchujo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ni Fiston Mayele.

Kwenye kikosi cha Yanga, Mayele ndiye kinara wa mabao kwenye Kombe la Afrika baada ya nyota huyo kutupia jumla ya mabao saba katika hatua zilizopita dhidi ya Zalan kutoka Sudan Kusini na Al Hilal ya Sudan.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Marchand amesema Mayele ni mchezaji mzuri ambaye anamfahamu kwa muda mrefu tangu akiitumikia AS Vita ya kwao DR Congo.

"Wakati nipo klabu nyingine kabla ya hii miaka miwili nyuma nilihitaji kumsajili kwa sababu alinivutia sana kutokana na aina ya uchezaji wake ila bahati mbaya sikufanikiwa kwa hilo." alisema Marchand.

Marchand aliongeza mbali na Mayele ila pia anawafahamu Tuisila Kisinda na Jesus Moloko japo Yanga ina wachezaji wazuri kutoka mataifa mbalimbali hivyo ni lazima wajiandae vizuri kutokana na ugumu wenyewe wa mchezo.