KMC yuaichapa Azam

Friday June 11 2021
kmc pic1
By Clezencia Tryphone

VIJANA wa KMC wameibugiza Azam Fc bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kujiweka fiti kuelekea michezo iliyosalia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo wa kirafiki uliopigwa leo asubuhi katika uwanja wa Chamazi nje ya Jiji la Dar es Salaam.

kmc pic

Beki Mrundi, Suleiman Ndikumana ndiye aliipatia bao KMC katika mchezo huo kwa mkwaju penalti.

Mkuu wa Idara ya habari ya KMC Christina Mwagala amesema mchezo huo kwao ulikuwa na maana kubwa sana kutokana na muda ambao timu iko bila mchezo.

"Tumecheza na Azam FC tumeshinda bao 1-0 ulikuwa mchezo mzuri sana kwetu na hata kwao pia,"

Advertisement

Amesema kwa sasa wakati ambao timu haina majukumu benchi la ufundi limeona litumie muda huu kucheza mchezo wa kirafiki

Advertisement