Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisubi Simba, Mkandala Yanga

Muktasari:

MTAANI kuna tetesi zinazomtaja kipa wa Tanzania Prisons, Jeremiah Kisubi kuwa anasubiri tu ligi imalizike kabla ya kutangazwa kuwa mchezaji wa Simba.

MTAANI kuna tetesi zinazomtaja kipa wa Tanzania Prisons, Jeremiah Kisubi kuwa anasubiri tu ligi imalizike kabla ya kutangazwa kuwa mchezaji wa Simba.

Akiwa na msimu bora na Wajelajela hao wa mkoani Mbeya ambao msimu huu wamehamia Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mechi mbili alizokaa langoni msimu huu dhidi ya Simba, Kisubi alichangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kuambulia alama ikiwemo mchezo walioshinda bao 1-0 na hizo zinatajwa kuwa chachu ya mabosi wa Simba kutaka awe kwenye kikosi chao msimu ujao.

Kelvin Frednand, meneja wa Prisons ambaye alikuwa jijini hapa na mchezaji wake Cleophas Mkandala, alipoulizwa kuhusu taarifa za wachezaji hao alisita kuthibitisha moja kwa moja kuhusu Kisubi kusajiliwa Simba.

‘‘Hizo taarifa za huyo mchezaji nimezisikia, ila kwa sasa siwezi kuthibitisha. Nachofahamu bado anamalizia mechi za Ligi Kuu zilizobaki hayo mengine yatafanyika au kuzungumzwa baada ya kumazilika kwa msimu huu,’’ alisema.

Kuhusu Mkandala, meneja huyo anayemsimamia kiungo huyo wa Dodoma Jiji, alisema ana ofa zinazosubiri kufanyiwa kazi na pande zinazomhitaji ikiwemo Yanga ambao wanatajwa kwa mara nyingine. Yanga msimu uliopita, walikaribia kumnasa kiungo huyo fundi, kabla ya dili kwenda mrama na kuibukia Dodoma Jiji.

“Kuna ishu za Yanga kumhitaji tena, huku pia tukiendelea kusubiri hatima ya timu ya nje ya nchi hii ambayo ndio tutaizingatia zaidi.”