Kisubi kuziba pengo la Mshery

BAADA ya tetesi nyingi hatimaye Mtibwa Sugar wamethibitisha kukamilisha mazungumzo na Simba kwaajili ya kunasa saini ya Jeremiah Kisubi ambaye ametolewa kwa mkopo na timu hiyo.

Kisubi alijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Tanzania Prisons ameitumikia Simba nusu msimu na sasa amejiunga na Mtibwa Sugar kwa mkopo.

Hata hivyo kama ambavyo Mwanaspoti iliwahi kuripoti kipa huyo kujiunga na walima miwa hao wa mkoani Morogoro, habari ilizopata leo zimethibitishwa rasmi baada ya mchezaji huyo kutambulishwa.

Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Swabri Aboubakari amesema tayari wamemalizana na kipa huyo tayari kuanza kuitumikia timu yao baada ya kumtambulisha leo.

Amesema wanaamini kujiunga kwa kipa huyo kutaziba bengo la aliyekuwa kipa wao namba moja Aboutwalib Mshery (21) aliyetimkia Yanga.

"Tumeshamaliza kila kitu na  Kisubi wakati huohuo tunaendelea na kukamilisha utaratibu wa wachezaji wengine ili kuungana na wenzao kikosini" amesema Aboubakari.